12
Maria Ampaka Isa Mafuta Huko Bethania
(Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9)
1 #
Yn 11:55; Mt 21:17 Siku sita kabla ya Pasaka, Isa alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Isa alikuwa anaishi. 2#Lk 10:38-42Wakaandaa karamu kwa heshima ya Isa. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Isa. 3#Yn 11:12Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja#12:3 Painti moja ni kama nusu lita. yenye manukato ya nardo#12:3 Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri. safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.
4 #
Mt 10:4
Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Isa, akasema, 5“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300#12:5 Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300. na fedha hizo wakapewa maskini?” 6#Yn 13:29Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.
7 #
Yn 19:40
Isa akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 8#Kum 15:11Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”
Shauri La Kumuua Lazaro
9 #
Yn 11:43, 44 Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Isa alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Isa, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Isa alikuwa amemfufua. 10#Lk 16:31Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 11#Yn 11:45; 12:18kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Isa na kumwamini.
Kuingia Kwa Isa Yerusalemu Kwa Ushindi
(Mathayo 21:1-11; Marko 1:1-11; Luka 19:28-40)
12 #
Mt 21:8; Mk 11:8; Lk 19:35, 36 Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Isa angekuja Yerusalemu. 13#Za 118:25-26; Yn 1:49Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema,
“Hosana!”#12:13 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.
“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
“Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
14 #
Mt 21:7
Isa akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,
15 #
Zek 9:9
“Usiogope, Ewe binti Sayuni;
tazama, Mfalme wako anakuja,
amepanda mwana-punda!”
16 #
Lk 18:34; Yn 7:39 Wanafunzi wake Isa mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Isa alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.
17 #
Yn 11:42
Wale waliokuwepo wakati Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia. 18#Yn 12:11; 19:37Ni kwa sababu pia walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu ndiyo maana umati wa watu ukaenda kumlaki. 19#Yn 11:47, 48Hivyo Mafarisayo walipoona hayo wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”
Isa Anatabiri Kifo Chake
20 #
Yn 7:35; Mdo 11:20 Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu. 21#Mt 11:21; Yn 1:44Hawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Isa.” 22Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Isa.
23 #
Yn 13:32; 17:1 Isa akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24#1Kor 15:36Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi. 25#Mk 8:35; Lk 14:26Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele. 26#Flp 1:23 Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.
27 #
Mt 26:38, 39; Lk 12:50; Yn 13:21; Lk 22:53; Yn 18:37 “Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii.’ Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu. 28#Mt 3:17Baba, litukuze jina lako.”
Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.” 29#Lk 22:43Ule umati wa watu uliokuwa mahali pale uliisikia nao ukasema, “Hiyo ni sauti ya radi,” wengine wakasema, “Malaika ameongea naye.”
30 #
Kut 19:9
Isa akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu. 31#Yn 16; 11; Efe 2:2; 1Yn 5:19Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 32#Isa 11:10; Yn 3:14; 6:44Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33#Yn 18:32; 21:19Isa aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa.
34 #
Za 110:4; Isa 9:7; Mt 8:20; Yn 3:14 Ule umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba ‘Al-Masihi#12:34 Al-Masihi maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu?’ Huyu ‘Mwana wa Adamu ni nani?’ ”
35 #
Yn 1:9; 8:12; 9:5; Yer 13:16; Efe 5:8; 1Yn 2:11 Ndipo Isa akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakokwenda. 36#Lk 16:8; Efe 5:8; 1The 5:5; 1Yn 2:9, 10, 11; Yn 8:59; 11:54Wekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Isa aliondoka, akajificha wasimwone.
Wayahudi Waendelea Kutokuamini
37 #
Yn 2:11
Hata baada ya Isa kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini. 38#Isa 53:1; Rum 10:16Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema:
“Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu,
na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?”
39 #
Isa 6:9, 10; Mt 13:14, 15 Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine:
40 #
Isa 6:10; Mt 13:13, 15 “Amewafanya vipofu,
na kuifanya mioyo yao kuwa migumu,
ili wasiweze kuona kwa macho yao,
wala kuelewa kwa mioyo yao,
wasije wakageuka nami nikawaponya.”
41 #
Isa 6:1-4; Lk 24:27 Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Isa na kunena habari zake.
42 #
Yn 7:48; 9:22 Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. 43#Yn 5:44; Rum 2:29Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
Amwaminiye Isa Hatabaki Gizani
44 #
Mt 10:40; Yn 5:24 Isa akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma. 45#Yn 14:9Yeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma. 46#Yn 3:19; Yn 8:12Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.
47 #
Yn 3:17
“Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa. 48#Yn 5:45Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. 49#Yn 14:31Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema. 50#Yn 8:26, 28Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”