Yohana 3
NMM

Yohana 3

3
Nikodemo Amwendea Isa Usiku
1 # Yn 7:50; 19:39; Lk 23:13 Basi palikuwa na mtu mmoja Farisayo, jina lake Nikodemo, mmoja wa Baraza la Wayahudi#3:1 Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo Baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. lililotawala. 2#Yn 2:11; 9:16, 33; Mdo 2:22; 10:38Huyu alimjia Isa usiku akamwambia, “Rabi, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye.”
3 # Yn 1:13; 1Pet 1:23 Isa akamjibu, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili.”
4Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!”
5 # Tit 3:5 Isa akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho. 6#Yn 1:13; Mwa 5:3; Za 51:5Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. 7Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ 8#Mk 4:41; Mhu 11:5Upepo huvuma popote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”
9 # Yn 6:52, 60 Nikodemo akamuuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”
10 # Lk 2:46 Isa akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli, nawe huelewi mambo haya? 11#Yn 1:18; 7:16-17Amin, amin ninakuambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu. 12#Lk 22:67Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni? 13#Mit 30:4; Efe 4:8-10; Ebr 4:14; 9:24Hakuna mtu yeyote aliyekwenda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. 14#Hes 21:8-9; Yn 8:28; 12:32Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu. 15#Mwa 15:6; Rum 3:22Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele.
16 # Rum 5:8; Efe 2:4; Yn 6:29, 40; Yn 11:25-26 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17#Yn 17:8, 21; Yn 20:21; Isa 53:11; Rum 11:14Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa. 18#Yn 5:24; 1:18; 1Yn 4:9Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19#Yn 1:4; Yn 8:12Hii ndiyo hukumu kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 20#Efe 5:11-13Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21Lakini yule aishiye kwa ukweli huja kwenye nuru, ili ionekane wazi kwamba matendo yake yametendeka katika Mungu.”
Ushuhuda Wa Yahya Mbatizaji Kuhusu Isa
22 # Yn 4:2 Baada ya haya, Isa na wanafunzi wake walikwenda katika nchi ya Uyahudi, nao wakakaa huko kwa muda na kubatiza. 23#1Sam 9:4; Mt 3:6Yahya naye alikuwa akibatiza huko Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. Watu wazima wakamjia huko ili kubatizwa. 24#Mt 4:12; Mt 14:3(Hii ilikuwa kabla Yahya hajatiwa gerezani). 25#Yn 2:6Mashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yahya na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa kwa utakaso. 26#Mt 23:7; Yn 1:7Wakamwendea Yahya wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!”
27 # Ebr 5:4; 1Kor 4:7; Yak 1:17 Yahya akawajibu, “Hakuna mtu yeyote awezaye kupata kitu chochote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni. 28#Yn 1:20-23; 3:9; Mt 9:15; Flp 2:2; 2Yn 1:12Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Al-Masihi,#3:28 Al-Masihi maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. ila nimetumwa nimtangulie.’ 29#Mt 22:2; 2Kor 11:2; Efe 5:25, 27; Ufu 21:9; Wim 5:1Bibi arusi ni wa bwana arusi. Lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama karibu naye na kusikiliza kutoka kwake, hufurahi sana aisikiapo sauti ya bwana arusi. Kwa sababu hii furaha yangu imekamilika. 30#2Sam 3:1Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.”
Yeye Aliyetoka Mbinguni
31 # Yn 8:23; 1Yn 4:5 “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. 32#Yn 8:26; Yn 15:15Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake. 33#Rum 3:4; 1Yn 5:10Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. 34#Isa 42:1; Mt 12:18Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo. 35#Mt 28:18; Yn 17:2Baba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi mwake. 36#Yn 5:24; 6:47Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu