12
Hotuba Ya Nne Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Mimi Ni Mtu Wa Kuchekwa
1Ndipo Ayubu akajibu:
2 #
Ay 15:8; 17:10 “Bila shaka ninyi ndio watu,
nayo hekima itakoma mtakapokufa!
3 #
Ay 13:2; 15:9 Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi;
mimi si duni kwenu.
Ni nani asiyejua mambo haya yote?
4 #
Mwa 6:9; 38:23; Ay 21:3; 15:16; Za 91:15 “Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu,
ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu:
mimi ni mtu wa kuchekwa tu,
ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia!
5 #
Za 123:4; 17:5; 37:31; 38:16; 66:9; 73:2; 94:18; Mit 14:2 Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba
kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza.
6 #
Ay 5:24; 22:18; 9:24 Hema za wanyang’anyi hazisumbuliwi,
wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama:
wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.
7 #
Ay 35:11; 18:3; Mt 6:26; Rum 1:20 “Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha,
au ndege wa angani, nao watawaambia;
8au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha,
au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.
9 #
Isa 41:20; 1:3; Ay 9:24 Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua
kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili?
10 #
Hes 16:22; Mdo 17:28; Dan 5:23 Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe,
na pumzi ya wanadamu wote.
11 #
Ay 34:3
Je, sikio haliyajaribu maneno
kama vile ulimi uonjavyo chakula?
12 #
1Fal 4:2; Ay 15:10; 17:4; 32:7, 9; 34:4, 10 Je, hekima haipatikani katikati ya wazee?
Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?
13 #
Mit 21:30; Isa 45:9; Yer 32:19; 1Kor 1:24; Dan 1:17 “Hekima na nguvu ni vya Mungu;
shauri na ufahamu ni vyake yeye.
14 #
Ay 16:9; 9:3; Kum 13:16; Eze 26:14; Ufu 3:7; Za 127:1; Isa 24:20; 25:2 Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena;
mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.
15 #
1Fal 8:35; Isa 40:12; Kum 28:22; Mwa 7:11, 14 Akizuia maji, huwa pana ukame;
akiyaachia maji, huharibu nchi.
16 #
2Nya 18:22; Rum 2:11; Ay 9:4; 13:7, 9; 27:4 Kwake kuna nguvu na ushindi;
adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.
17 #
Ay 12:19; 19:9; Isa 20:4; Ay 3:14; 1Kor 1:20 Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara,
naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.
18 #
Za 107:14; 116:16; Nah 1:13; Ay 12:21; 34:18 Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme,
na kuwafunga mishipi ya kiunoni.
19 #
Dan 2:21, 34; Kum 24:15; Ay 9:24; 14:20; 22:8; 24:12, 22; 12:17; Isa 2:22 Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara,
na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.
20 #
Yer 32:9; Kum 4:33-34; Ay 12:12, 24; Dan 4:33-34 Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika,
na kuondoa busara ya wazee.
21 #
Ay 12:18; 3:15; Isa 34:12 Huwamwagia dharau wanaoheshimika,
na kuwavua silaha wenye nguvu.
22 #
1Kor 4:5; Ay 3:5; Za 139:12; Dan 2:22 Hufunua mambo ya ndani ya gizani,
na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.
23 #
Isa 13:4; 54:3; Kut 34:24; Mt 10:26 Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza;
hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.
24Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao;
huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia.
25 #
Kum 28:29; Ay 5:14; Za 107:27; Isa 24:20 Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga;
huwafanya wapepesuke kama walevi.