14
1 #
Mhu 2:23; Mwa 3:17; Ay 15:14; 10:20; Mt 11:11; Za 51:5 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke
siku zake ni chache nazo zimejaa taabu.
2 #
Za 103:15; Yak 1:10; 1Pet 1:24; Isa 40:6-8; Mhu 6:12 Huchanua kama ua kisha hunyauka;
huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu.
3 #
Za 144:3; 8:4; 143:2; Ay 7:18 Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo?
Je, utamleta mbele yako katika hukumu?
4 #
Mwa 5:3; Ay 4:17; Za 51:10; Rum 5:12; Efe 2:1-3; Yn 3:6 Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi?
Hakuna awezaye!
5 #
Ay 24:1; 21:21; Za 31:15; 139:16; 39:4; 90:12; Mdo 17:26 Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka;
umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake
na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka.
6 #
Ay 7:19; 7:1, 2; Za 39:13; Isa 16:14; 21:16 Hivyo angalia mbali umwache,
hadi awe amekamilisha muda wake
kama mtu aliyeajiriwa.
7 #
Ay 19:10; 24:20; Za 52:5; Isa 11:1; 53:2; 60:21; 6:13 “Kwa maana lipo tumaini kwa mti;
kama ukikatwa utachipuka tena,
nayo machipukizi yake mapya hayatakoma.
8 #
Isa 6:13; 11:1; 53:2 Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini
na kisiki chake kufa udongoni,
9 #
Ay 29:9; Zek 10:1; Za 1:3; Yer 17:8; Eze 31:7; Law 26:4; Eze 34:27 lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua
na kutoa machipukizi kama mche.
10 #
Ay 14:12; 10:21; 13:19 Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake;
hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena!
11 #
2Sam 14:14; Isa 19:5 Kama vile maji yatowekavyo katika bahari,
au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu,
12 #
Za 102:26; Ufu 21:1; Mdo 3:21; Ay 14:10; Ufu 20:11 ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke;
hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena,
wanadamu hawataamka au kuamshwa
kutoka kwenye usingizi wao.
13 #
Za 30:5; Isa 54:7; Ay 6:8; 7:9; Isa 26:20; 54:7; Mwa 8:1 “Laiti kama ungenificha kaburini,#14:13 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
na kunisitiri hadi hasira yako ipite!
Laiti ungeniwekea wakati,
na kisha ukanikumbuka!
14 #
Ay 7:1; 2Fal 6:33; Za 16:10; 1Kor 15:42-58; Flp 3:21 Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena?
Siku zote za kazi zangu ngumu
nitangojea kufanywa upya kwangu.
15 #
Ay 13:22; Yn 5:28; 1The 4:16; Za 50:4 Utaniita nami nitakuitika;
utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.
16 #
Mit 5:21; Yer 16:17; 32:19; Hos 13:12; 1Kor 13:5 Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu,
lakini hutazifuatia dhambi zangu.
17 #
Kum 32:34; Ay 13:23; 9:30; Yer 32:10 Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko,
nawe utazifunika dhambi zangu.
18 #
Eze 38:20; Ay 18:4 “Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika
na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake,
19 #
Eze 13:13; Mwa 7:23; Ay 7:8 kama maji yamalizavyo mawe,
na mafuriko yachukuavyo udongo,
ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu.
20 #
Ay 4:20; 7:10; 8:18; 12:19; 27:19; Yak 1:10 Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka;
waibadilisha sura yake na kumwondoa.
21 #
Mhu 9:5; Isa 63:16; 1Sam 4:20 Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu;
kama wakidharauliwa, yeye haoni.
22 #
Za 38:7; Isa 21:3; Yer 4:19; Ay 21:21 Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe,
naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.”