15
Elifazi Anaongea: Ayubu Anadhoofisha Imani
1 #
Ay 4:1
Kisha Elifazi Mtemani akajibu:
2 #
Mwa 41:6; Ay 6:26 “Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu,
au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki?
3 #
Neh 4:2-3; Ay 6:26 Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa,
kwa hotuba zisizo na maana?
4 #
Ay 25:6
Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu
na kuzuia ibada mbele za Mungu.
5 #
Ay 11:6; 22:5; 5:13; Mt 16:23 Dhambi yako inasukuma kinywa chako,
nawe umechagua ulimi wa hila.
6 #
Za 10:2; Mt 12:37; Lk 19:22; Ay 7:15; 18:7 Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu;
midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako.
7 #
Ay 38:21; 1Sam 2:8; Mit 8:25; Za 90:2 “Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa?
Ulizaliwa kabla ya vilima?
8 #
Yer 23:18; 1Kor 2:11 Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu?
Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?
9 #
Ay 12:3
Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi?
Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?
10 #
Ay 12:12; 32:6-7; 8:8-10 Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu,
watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako.
11 #
Mwa 37:35; 2Kor 1:3-4; Kum 8:3; Yer 15:16 Je, faraja za Mungu hazikutoshi,
au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu?
12 #
Ay 11:13; 36:13 Kwa nini moyo wako unakudanganya,
na kwa nini macho yako yanang’aa,
13 #
Mit 29:11; Dan 11:30; Za 94:4; Ay 11:8; 22:5; 30:2 ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu,
na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako?
14 #
Ay 14:1; 4:17; 2Nya 6:36; Mhu 7:18, 20 “Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi,
au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?
15 #
Ay 5:1; 4:18 Kama Mungu hawaamini watakatifu wake,
kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake,
16 #
Law 5:2; Ay 12:4; 20:12; Mit 19:28; Za 14:1 sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu,
ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji!
17 #
Ay 4:8
“Nisikilize mimi nami nitakueleza,
acha nikuambie yale niliyoyaona,
18 #
Kum 32:7; Ay 8:8; Mwa 18:19 ambayo watu wenye hekima wameyanena,
bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao
19 #
Mwa 12:1; Ay 22:8 (wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi,
hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao):
20 #
Oba 1:15; Sef 1:17 Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso,
miaka yote aliwekewa mkorofi.
21 #
1Sam 3:11; Yer 6:25; Isa 13:3; 1The 5:3 Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake;
katika kufanikiwa kwake, wanyang’anyi humshambulia.
22 #
Hos 9:13; Amo 5:19 Hukata tamaa kuokoka gizani;
amewekwa kwa ajili ya upanga.
23 #
Za 59:15; 109:10; Ay 18:12 Hutangatanga, akitafuta chakula;
anajua kwamba siku ya giza iko karibu.
24 #
Isa 8:22; 9:1; Ay 15:20; 18:14 Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu;
humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita,
25 #
Za 2:2-3; Mit 21:30 kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake
na kujigamba dhidi ya Mwenyezi,
26 #
Yer 44:16
kwa kiburi akishambulia dhidi ya Mungu
akiwa na ngao nene, iliyo imara.
27 #
Amu 3:17; Za 17:10 “Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unene
na kiuno chake kimevimba kwa kunenepa,
28 #
Isa 5:9; Ay 3:14 ataishi katika miji ya magofu,
na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote,
nyumba zinazokuwa vifusi.
29 #
Ay 3:15; 7:8; Isa 5:8 Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu,
wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi.
30 #
Ay 4:9, 15; 16:7; 20:26; Kut 15:10 Hatatoka gizani;
mwali wa moto utanyausha machipukizi yake,
nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali.
31 #
Yer 7:4-8; Mt 6:19; Za 62:10 #
Ay 31:5; Mit 1:16; 6:18; Isa 44:20; 59:7; Mik 2:11; Mk 13:5 Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili,
kwa kuwa hatapata malipo yoyote.
32 #
Mhu 7:17; Za 109:8; Mit 10:27; Ay 18:16 Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake,
nayo matawi yake hayatastawi.
33 #
Hab 3:17
Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva,
kama mzeituni unaodondosha maua yake.
34 #
Kut 23:8; Ay 8:22; Isa 33:14 Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa,
nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa.
35 #
Hos 10:13; Gal 6:7; Za 7:14 Hutunga mimba ya madhara na kuzaa uovu;
matumbo yao huumba udanganyifu.”