16
Hotuba Ya Tano Ya Ayubu
Ayubu Anathibitisha Tena Hali Yake Ya Kutokuwa Na Hatia
1Kisha Ayubu akajibu:
2 #
Ay 6:15; 13:4; Za 69:20 “Nimepata kusikia mambo mengi kama haya,
nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha!
3 #
Ay 6:26; 11:2; 18:2 Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho?
Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno?
4 #
Mt 27:29; Yer 18:16; Mao 2:15 Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi,
kama mngekuwa katika hali yangu;
ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu,
na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
5 #
Ay 29:25; Mwa 37:35 Lakini kinywa changu kingewatia moyo;
faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.
6 #
Ay 6:3; 7:21 “Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi;
nami kama nikijizuia, wala hayaondoki.
7 #
Amu 8:5; Ay 7:3; 1:19 Ee Mungu, hakika umenichakaza;
umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.
8 #
Mao 5:17; Ay 10:17; 17:7; 19:20; Za 22:17; 88:9; 6:7 Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi;
nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu.
9 #
Ay 12:14; 13:24; Mao 2:16; Mdo 7:54; Hos 6:1; Ay 30:21; 9:5; 18:4; 19:11 Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake,
na kunisagia meno yake;
adui yangu hunikazia macho yake makali.
10 #
Za 22:13; Mao 3:30; Mdo 7:57; 23:2; Za 27:3; Mik 5:1 Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki;
hunipiga shavuni mwangu kwa dharau,
na kuungana pamoja dhidi yangu.
11 #
Ay 9:24
Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya,
na kunitupa katika makucha ya waovu.
12 #
Ay 9:17; 6:4; Mao 3:12 Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja;
amenikamata shingo na kuniponda.
Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;
13 #
Mit 7:23; Mao 3:13 wapiga upinde wake wananizunguka.
Bila huruma, huchoma figo zangu,
na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.
14 #
Ay 9:17; 10:3; Yoe 2:7 Huniponda tena na tena;
hunishambulia kama shujaa wa vita.
15 #
Mwa 37:34; Ay 2:8 “Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu
nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi.
16 #
Ay 16:20; 2:7; 17:7; 30:17, 30; Isa 52:14; Za 6:6 Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia,
macho yangu yamepigwa na giza kuu.
17 #
Yer 18:11; Yon 3:8 Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri,
na maombi yangu ni safi.
18 #
Mwa 4:10; Ay 27:9; Isa 26:21; Za 66:18-19; Ebr 11:4 “Ee nchi, usiifunike damu yangu,
nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe.
19 #
Mwa 31:50; Rum 1:9; 1The 2:5; Ay 22:12; 19:27; Za 113:5; Isa 33:5 Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni;
wakili wangu yuko juu.
20 #
Mao 2:19; Rum 8:34; Yn 15:15; Ay 16:16 Mwombezi wangu ni rafiki yangu
macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu;
21 #
1Fal 8:45; Za 140:12 kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu
kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake.
22 #
Ay 10:21; Mhu 12:5 “Ni miaka michache tu itapita
kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.