17
1 #
Za 88:3-4; Mhu 12:1-7 Moyo wangu umevunjika,
siku zangu zimefupishwa,
kaburi linaningojea.
2 #
1Sam 1:6-7; Ay 11:3 Hakika wenye mizaha wamenizunguka;
macho yangu yamebaki kutazama uadui wao.
Ayubu Anaomba Msaada
3 #
Za 35:27; 40:17; Mit 6:1; Isa 38:14 “Ee Mungu, nipe dhamana unayodai.
Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu?
4 #
Ay 12:12
Umezifunga akili zao zisipate ufahamu,
kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.
5 #
Kut 22:15; Ay 11:20 Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira,
macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
6 #
1Fal 9:7; Yer 15:4 “Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu,
mtu ambaye watu humtemea mate usoni.
7 #
Ay 16:8; 2:12; 16:16 Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi;
umbile langu lote ni kama kivuli.
8 #
Kut 4:14; Ay 22:19 Watu wanyofu wanatishwa na hili;
watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu.
9 #
Mit 4:18; 2Sam 22:21; Ay 22:30 Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao,
nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu.
10 #
Ay 12:3
“Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena!
Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu.
11 #
Ay 17:15; Isa 38:10; Ay 7:6 Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika,
vivyo hivyo shauku za moyo wangu.
12 #
Isa 50:11; Ay 5:17-26; 11:17 Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana,
kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’
13 #
2Sam 14:14; Ay 3:13; Za 139:8; 88:18 Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi,#17:13 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
kama nikikitandika kitanda changu gizani,
14 #
Ay 13:28; 30:28, 30; 4:19; 7:5; Za 16:10; 49:9; 17:15; Ay 7:6; Za 31:23; Mao 3:18; Eze 37:11 kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’
na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’
15liko wapi basi tarajio langu?
Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?
16 #
Mwa 2:7; Yon 2:6; Ay 3:17 Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti?#17:16 Malango ya mauti hapa ina maana ya Kuzimu.
Je, tutashuka pamoja mavumbini?”