18
Bildadi Anasema: Mungu Huwaadhibu Waovu
1 #
Ay 8:1
Bildadi Mshuhi akajibu:
2 #
Ay 8:2; 16:3 “Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya?
Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea.
3 #
Za 73:22; Ay 12:7 Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama,
na kuonekana wajinga machoni pako?
4 #
Ay 13:14; 16:9; 14:18 Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande
katika hasira yako,
je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe?
Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?
5 #
Yer 25:10; Yn 8:12; Mit 13:9 “Taa ya mwovu imezimwa,
nao mwali wa moto wake umezimika.
6 #
Ay 8:22; 5:14; 11:17; 12:25 Mwanga hemani mwake umekuwa giza;
taa iliyo karibu naye imezimika.
7 #
Za 18:36; Mit 4:12; Ay 5:13; 15:6 Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa;
shauri lake baya litamwangusha.
8 #
Mik 7:2; Hab 1:15 Miguu yake imemsukumia kwenye wavu,
naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
9 #
Ay 22:10; 30:12; Isa 24:18; Yer 48:44; Amo 5:14; Mit 7:22 Tanzi litamkamata kwenye kisigino;
mtego utamshikilia kwa nguvu.
10 #
Mit 7:22; Isa 51:20; 1Sam 28:9; Za 140:5 Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake;
mtego uko kwenye njia yake.
11 #
Ay 15:21; 20:8; Za 31:13; Isa 22:18; Yer 6:25 Vitisho vimemtia hofu kila upande,
na adui zake humwandama kila hatua.
12 #
Isa 9:20; 65:13; 8:21; Ay 21:17; 31:3; 15:25 Janga linamwonea shauku;
maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
13 #
Zek 14:12; Hes 12:12 Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake;
mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
14 #
Ay 8:22; 15:24; 18:11 Atang’olewa kutoka usalama wa hema lake,
na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
15 #
Mwa 19:24; Za 11:6; Ay 18:18; 20:26 Moto utakaa katika hema lake;
moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
16 #
Hos 5:12; Amo 2:9; Mwa 27:28 Mizizi yake chini itakauka
na matawi yake juu yatanyauka.
17 #
Mit 2:22; 10:7; Isa 49:15; Kum 32:26; 9:14; Za 9:5; 69:28 Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia,
wala hatakuwa na jina katika nchi.
18 #
Ay 5:14; 18:11; 11:20; 30:8 Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani,
naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
19 #
Za 37:28; 21:10; Isa 14:22; Ay 27:14-15 Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake,
wala aliyenusurika mahali alipoishi.
20 #
Yer 46:21; Eze 7:7 Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata;
watu wa mashariki watapatwa na hofu.
21 #
Ay 21:28; Yer 9:3; 1The 4:5 Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu;
ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”