Ayubu 19
NMM

Ayubu 19

19
Hotuba Ya Sita Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Najua Mkombozi Wangu Yu Hai
1Ndipo Ayubu akajibu:
2 # 1Sam 1:6; Za 6:2, 3; Ay 6:9; 13:25 “Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini,
na kuniponda kwa maneno yenu?
3 # Mwa 31:7; Ay 20:3 Mara kumi hizi mmenishutumu;
bila aibu mnanishambulia.
4 # Ay 6:24; Za 19:12; Eze 18:4 Kama ni kweli nimepotoka,
kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.
5 # Za 38:16; 55:12; Mik 7:8 Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu,
na kutumia unyonge wangu dhidi yangu,
6 # Ay 6:29; 18:8; 10:3 basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya,
naye amekokota wavu wake kunizunguka.
7 # Ay 9:24; 30:20; Za 22:2; Hab 1:2-4 “Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu;
ingawa ninaomba msaada, hakuna haki.
8 # Mao 3:7; Hos 2:6; Mhu 6:4; Yer 14:19 Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita;
ameyafunika mapito yangu na giza.
9 # Ay 12:17; Za 89:39-44; Mao 5:16 Amenivua heshima yangu,
na kuniondolea taji kichwani pangu.
10 # Ay 12:14; 7:6; 14:7 Amenibomoa kila upande hadi nimeisha;
ameling’oa tegemeo langu kama mti.
11 # Ay 16:9; 13:14 Hasira yake imewaka juu yangu;
amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.
12 # Ay 16:13; 16:10; 3:23 Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu;
yamenizingira,
yamepiga kambi kulizunguka hema langu.
13 # Ay 16:10-13; 30:12; Mt 26:56; 2Tim 4:16 “Amewatenga ndugu zangu mbali nami;
wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa.
14 # Ay 19:19; 2Sam 15:12; Ay 12:4; 16:20; Za 88:18; Yer 20:10; 38:22 Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali;
rafiki zangu wamenisahau.
15 # Mwa 14:14; Mhu 2:7 Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni;
wananitazama kama mgeni.
16Namwita mtumishi wangu, wala haitiki,
ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe.
17 # Za 38:5 Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu;
nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe.
18 # 2Fal 2:23; Ay 13:25 Hata watoto wadogo hunidhihaki;
ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.
19 # Za 38:11; 55:12-13; Ay 3:10 Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa;
wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.
20 # Ay 2:5 Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu;
nimeponea nikiwa karibu kufa.
21 # Ay 6:14; Amu 2:15; Ay 4:5; 10:3; Mao 3:1 “Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma,
kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga.
22 # Ay 13:25; 16:11; Mit 30:14; Isa 53:4 Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo?
Hamtosheki kamwe na mwili wangu?
23 # Kut 17:16; Isa 30:8 “Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu,
laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu,
24 # Yer 17:1; Ay 16:18 kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma,
au kuyachonga juu ya mwamba milele!
25 # Law 25:25; Mit 23:11; 1Sam 14:39; Ay 16:19 Ninajua kwamba Mkombozi#19:25 Au: Mtetezi. wangu yu hai,
naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.
26 # Hes 12:8; 1Yn 3:2 Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa,
bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;
27 # Lk 2:30; Za 42:1; 63:1; 54:2 mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe:
mimi, wala si mwingine.
Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!
28“Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda,
maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’
29 # Ay 15:22; Za 58:11; Mhu 12:14 ninyi wenyewe uogopeni upanga,
kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga,
nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu