Ayubu 20
NMM

Ayubu 20

20
Sofari Anasema: Uovu Hupokea Malipo Ya Haki
1 # Ay 2:11 Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu:
2 # Za 42:5; Mao 1:20 “Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu,
kwa sababu nimehangaika sana.
3 # Ay 19:3 Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima,
nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu.
4 # Kum 4:32; Ay 32:7 “Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani,
tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani,
5 # Ay 8:12; Za 73:19; 37:35 macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi,
nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.
6 # Ay 33:17; Isa 16:6; Mwa 11:4; Isa 14:13-14; Oba 1:3-4 Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni
na kichwa chake hugusa mawingu,
7 # Ay 4:20; 7:8; 14:20 ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe.
Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’
8 # Za 90:5; 73:20; Mhu 6:12; 12:7; Ay 18:11-18; Isa 17:14; 29:7 Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena,
amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.
9 # Ay 7:8 Jicho lililomwona halitamwona tena;
mahali pake hapatamwona tena.
10 # Ay 5:4; 20:15, 18, 20; 3:15 Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini,
nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyang’anya watu.
11 # Ay 13:26; 21:24; Ay 17:16 Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake,
zitalala naye mavumbini.
12 # Ay 15:16; Za 10:7; 140:3 “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake
naye huuficha chini ya ulimi wake,
13 # Hes 11:18-20 ingawa hawezi kukubali kuuachia uende,
lakini huuweka kinywani mwake.
14 # Za 104:26; Ay 10:18; Mwa 1:21; Ay 41:1, 8, 10, 25 # Mit 20:17; Yer 2:19; 4:18; Ufu 10:9; Hes 21:6 Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake,
nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
15 # Ay 20:10; Law 18:25 Atatema mali alizozimeza;
Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.
16 # Kum 32:24, 34 Atanyonya sumu za majoka;
meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
17 # Kum 32:13-14; Ay 29:6; Yer 17:6 Hatafurahia vijito,
mito inayotiririsha asali na siagi.
18 # Ay 20:10; 5:5; Za 109:11 Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila;
hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.
19 # Kum 15:11; Amo 8:4 Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu;
amenyang’anya kwa nguvu nyumba asizozijenga.
20 # Mhu 5:12-14 “Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana;
hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.
21 # Ay 7:8 Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale;
kufanikiwa kwake hakutadumu.
22 # Amu 2:15; Lk 2:16-20; Ay 20:29; 21:17, 30; 31:2-3 Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata;
taabu itamjia kwa nguvu zote.
23 # Za 78:30-31 Atakapokuwa amelijaza tumbo lake,
Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake,
na kumnyeshea mapigo juu yake.
24 # Yer 46:21; Amo 5:19; Isa 24:18 Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma,
mshale wa shaba utamchoma.
25 # Ay 18:11; 16:13; Za 88:15-16 Atauchomoa katika mgongo wake,
ncha ing’aayo kutoka ini lake.
Vitisho vitakuja juu yake;
26 # Ay 5:14; 1:16; 15:34; 26:6; 28:22; 31:12; Za 21:9 giza nene linavizia hazina zake.
Moto usiopepewa na mtu utamteketeza,
na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.
27 # Kum 31:28; Isa 26:21 Mbingu zitaweka wazi hatia yake,
nayo nchi itainuka kinyume chake.
28 # Kum 28:31; Mt 7:26-27; Hes 14:28-32; Efe 5:6 Mafuriko yataichukua nyumba yake,
maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.
29 # Yer 13:25; Kum 29:20, 28; Ufu 21:8; Mt 24:51 Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu,
urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu