21
Hotuba Ya Saba Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Waovu Mara Nyingi Huenda Bila Kuadhibiwa
1Ndipo Ayubu akajibu:
2 #
Ay 13:17; 21:34 “Yasikilizeni maneno yangu kwa makini;
hii na iwe faraja mnayonipa mimi.
3 #
Ay 6:14; 11:3; 16:10 Nivumilieni ninapozungumza,
nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki.
4 #
Za 22:1-3; Ay 6:3, 11; 1Sam 1:16 “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu?
Kwa nini nisikose subira?
5 #
Amu 18:19; Ay 40:4 Niangalieni mkastaajabu;
mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu.
6 #
Mwa 45:3; Ay 4:14 Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa,
nao mwili wangu unatetemeka.
7 #
Mhu 7:15; Mal 3:15; Yer 12:1-3 Kwa nini waovu wanaendelea kuishi,
wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu?
8 #
Za 17:14; Mal 3:15 Huwaona watoto wao wakithibitika
wakiwa wamewazunguka,
wazao wao mbele za macho yao.
9 #
Ay 5:24; Za 73:5 Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu;
fimbo ya Mungu haiko juu yao.
10 #
Kut 23:26
Madume yao ya ng’ombe huvyaza bila kushindwa kamwe;
ng’ombe wao huzaa wala hawaharibu mimba.
11 #
Za 78:52; 107:41 Huwatoa watoto wao nje kama kundi;
wadogo wao huchezacheza.
12 #
1Nya 15:16; Mt 15:17 Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi,
nao huifurahia sauti ya filimbi.
13 #
Ay 24:19; Za 49:14; Isa 14:15; Ay 3:13 Huitumia miaka yao katika mafanikio
nao hushuka kaburini kwa amani.
14 #
Ay 4:17; Kum 32:15; Isa 30:11; 1Sam 11:15 Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’
Hatuna haja ya kufahamu njia zako.
15 #
Yer 9:6; Mal 3:14 Mwenyezi ni nani hata tumtumikie?
Tutapata faida gani kumwomba?
16 #
Ay 22:18; Za 1:1; 26:5; 36:1 Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe,
hivyo najitenga mbali na shauri la waovu.
17 #
Ay 18:5; 18:12; 20:22, 28 “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa?
Ni mara ngapi maafa huwajia,
yale yawapatayo ambayo Mungu
huwapangia katika hasira yake?
18 #
Ay 13:15; Mwa 19:15; Ay 7:10; Mit 10:25; Mwa 7:23 Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo,
kama makapi yachukuliwayo na dhoruba?
19 #
Kut 20:5; Yn 9:2 Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu
kwa ajili ya wanawe.’
Mungu na amlipe mtu mwenyewe,
ili apate kulijua!
20 #
Ay 6:4; Isa 51:17; Yer 25:15; Ufu 14:10 Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake;
yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi.
21 #
Ay 14:22; 14:5; 14:21; Mhu 9:5-6 Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma,
miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho?
22 #
Za 94:12; 86:8; Rum 11:34 “Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa,
iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote?
23 #
Mwa 15:15; Ay 13:26; 3:13 Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili,
akiwa salama na mwenye raha kamili,
24 #
Mit 3:8
mwili wake ukiwa umenawiri,
nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake.
25 #
Ay 10:1
Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi,
akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri.
26 #
Mhu 9:2-3; Isa 14:11 Hao wote hulala mavumbini,
nao mabuu huwafunika wote.
27“Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri,
mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya.
28 #
Ay 1:3; 12:21; 29:25; 31:37; 8:22 Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu,
mahema ambayo watu waovu walikaa?’
29Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri?
Je, hamkutafakari taarifa zao:
30 #
Ay 31:3; Mit 16:4; Isa 5:30; Rum 5:2 kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa,
kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu?
31 #
Ay 34:11; Za 62:12; Mit 24:11-12; Isa 59:18 Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake?
Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda?
32 #
Isa 14:18
Hupelekwa kaburini,
nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake.
33 #
Ay 3:17-19; 17:16; 24:24 Udongo ulio bondeni ni mtamu kwake;
watu wote watamfuata,
nao umati wa watu usiohesabika umemtangulia.
34“Hivyo ninyi mnawezaje kunifariji kwa upuzi wenu?
Hakuna kilichosalia cha majibu yenu isipokuwa uongo!”