Ayubu 22
NMM

Ayubu 22

22
Elifazi Anasema: Uovu Wa Ayubu Ni Mkubwa
1 # Ay 4:1 Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:
2 # Lk 17:10; Za 16:2 “Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu?
Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi?
3 # Isa 1:11; Hag 1:8; Za 143:2; Ay 35:7; Za 9:12 Je, Mwenyezi angefurahia nini
kama ungekuwa mwadilifu?
Au je, yeye angepata faida gani
kama njia zako zingekuwa kamilifu?
4 # Isa 3:14; Eze 20:35 “Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea
na kuleta mashtaka dhidi yako?
5 # Ezr 9:13; Ay 11:6; Ezr 9:13; Ay 15:5; 15:13; 20:29; 29:17 Je, uovu wako si mkuu?
Dhambi zako si hazina mwisho?
6 # Kum 24:6, 17; Eze 18:12-16 Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu;
umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi.
7 # Ay 31:16-17; Eze 18:7; Mt 25:42 Hukumpa maji aliyechoka,
nawe ulimnyima chakula mwenye njaa,
8 # Ay 15:19; Isa 3:3; 5:13; 9:15; Ay 12:19 ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi:
mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake.
9 # Isa 10:2; Lk 1:53 Umewafukuza wajane mikono mitupu
na kuzivunja nguvu za yatima.
10 # Ay 18:9; 10:3; 15:21 Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote,
hatari ya ghafula inakutia hofu,
11 # Ay 5:14; Isa 58:10-11; Mao 3:54 ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona,
tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika.
12 # Ay 11:8; 16:19 “Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu?
Juu kuliko nyota zilizo juu sana!
13 # Eze 9:9; Efe 6:2; Sef 1:12; Za 139:11 Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’
Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo?
14 # Ay 26:9; Za 97:2; 105:39; 105:13; 2Fal 21:16; Ay 37:18; Za 18:11; Mit 8:27; Yer 23:23-24 Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi
atembeapo juu ya anga la dunia.
15 # Mwa 6:11-13 Je, utaifuata njia ya zamani,
ambayo watu waovu waliikanyaga?
16 # Ay 15:32; Mwa 7:23; Mt 7:26-27 Waliondolewa kabla ya wakati wao,
misingi yao ikachukuliwa na mafuriko.
17 # Ay 21:15 Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi!
Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’
18 # Ay 12:6; 21:16 Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri,
hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu.
19 # Za 64:10; 97:12; Ay 21:3 “Wenye haki wanaona maangamizi yao na kufurahi,
nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema,
20 # Ay 15:30 ‘Hakika adui zetu wameangamizwa,
nao moto umeteketeza mali zao.’
21 # Mit 3:10; 1Pet 5:6; Isa 27:5 “Mjue sana Mungu ili uwe na amani,
ndipo mema yatakapokujia.
22 # Kum 8:3; Ay 6:10; Eze 3:10; Mit 2:6; Za 37:31 Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake,
na maneno yake uyaweke moyoni mwako.
23 # Isa 19:22; 44:22; Eze 18:32; Mdo 20:32; Ay 11:14 Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya:
Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako,
24 # Isa 2:20; 30:22 kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi,
dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni,
25 # 2Fal 18:7; Mt 6:20-21 ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako,
naye atakuwa fedha yako iliyo bora.
26 # Za 2:8; Isa 61:10 Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi,
nawe utamwinulia Mungu uso wako.
27 # Ay 5:27; Isa 58:9 Utamwomba yeye, naye atakusikia,
nawe utazitimiza nadhiri zako.
28 # Za 103:11; 145:19; Ay 33:28; Mit 4:18; Za 97:11 Utakusudia jambo nalo litatendeka,
nao mwanga utaangazia njia zako.
29 # Za 18:27; 1Pet 5:5 Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’
ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo.
30 # 2Sam 22:21; Ay 42:7-8 Atamwokoa hata yule ambaye ana hatia,
ataokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu