23
Hotuba Ya Nane Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Kulalamika Kwangu Ni Uchungu
1Ndipo Ayubu akajibu:
2 #
Ay 6:3; 7:11; 1Sam 1:10 “Hata leo malalamiko yangu ni chungu;
mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua.
3 #
Kum 4:29
Laiti ningefahamu mahali pa kumwona;
laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!
4 #
Ay 13:18; 9:15 Ningeliweka shauri langu mbele zake,
na kukijaza kinywa changu na hoja.
5Ningejua kwamba angenijibu nini,
na kuelewa lile ambalo angelisema.
6 #
Ay 9:4, 19; Isa 27:4 Je, angenipinga kwa nguvu nyingi?
La, asingenigandamiza.
7 #
Mwa 3:8; Ay 9:3 Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake,
nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.
8“Lakini nikienda mashariki, hayupo;
nikienda magharibi, simpati.
9 #
Ay 9:11
Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni;
akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.
10 #
Za 66:10; 139:1-3; 12:6; 1Pet 1:7; Yak 1:12 Lakini anaijua njia niiendeayo;
akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
11 #
Za 17:5; Ay 31:7; Yer 11:20; Za 44:18; 125:5 Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu;
nimeishika njia yake bila kukengeuka.
12 #
Ay 6:10; 15:11; Yn 4:32, 34; Mt 4:4 Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake;
nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.
13 #
Za 115:3; Isa 55:11; Mhu 3:14; Rum 9:19 “Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga?
Yeye hufanya lolote atakalo.
14 #
1The 3:3; 1Pet 4:12 Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu,
na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.
15 #
Mwa 45:3; Yos 24:14; Mhu 3:14; 12:13; 2Kor 5:11 Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake;
nifikiriapo haya yote ninamwogopa.
16 #
Za 22:14; Yer 51:46; Ay 27:2 #
Kum 20:3; Ay 27:2; Kut 3:6; Ufu 6:16 Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia;
yeye Mwenyezi amenitia hofu.
17 #
Ay 3:6; 6:9; 19:8 Hata hivyo sijanyamazishwa na giza,
wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.