Ayubu 24
NMM

Ayubu 24

24
Ayubu Analalamikia Jeuri Duniani
1 # Yer 46:10; 2Pet 3:7; Ay 15:20; Mdo 1:7 “Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu?
Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio?
2 # Kum 19:14; 27:17; Mit 23:10 Watu husogeza mawe ya mpaka;
huchunga makundi ya wanyama waliyonyang’anya kwa nguvu.
3 # Kum 24:6-10; 12:17; Ay 6:27 Huwanyang’anya yatima punda wao,
na kumchukua rehani fahali wa mjane.
4 # Mit 28:28; Ay 20:19; Isa 11:4; Za 12:5 Humsukuma mhitaji kutoka njia,
na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha.
5 # Mwa 16:12; Za 104:23; Ay 30:3 Kama punda-mwitu jangwani,
maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula;
mahali palipo jangwa
huwapa chakula cha watoto wao.
6 # Ay 6:5; Rut 2:22; 1Fal 21:19 Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo
katika mashamba ya mizabibu ya waovu.
7 # Kut 22:26-27; Kum 24:12; Ay 22:6 Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi;
hawana chochote cha kujifunika baridi.
8 # Dan 4:25, 33; Mao 4:5 Hutota kwa mvua za mlimani,
nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri.
9 # Kum 24:17 Mtoto yatima hupokonywa matitini;
mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni.
10 # Kum 24:12-13; Law 19:9 Kwa kukosa nguo, hutembea uchi;
hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa.
11 # Isa 5:2; 16:10; Hag 2:16; Mik 6:15 Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia;
hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu.
12 # Isa 30:19; Ay 9:23; Ufu 6:10; Mhu 8:11 Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini,
nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada.
Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote
kwa kutenda mabaya.
13 # Ay 38:15; 1The 5:4-5; Za 18:28; Efe 5:8-14 “Wako wale wanaoiasi nuru,
wasiofahamu njia zake
wala hawakai katika mapito yake.
14 # Isa 3:15; Mik 3:3; Ay 20:19; Za 37:32; 10:9 Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka
naye huwaua maskini na mhitaji;
wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi.
15 # Mit 7:8-9; Za 10:11 Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza,
naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’
naye huuficha uso wake.
16 # Kut 22:2; Mt 6:19; Yn 3:20 Katika giza, huvunja majumba,
lakini wakati wa mchana hujifungia ndani;
hawataki kufanya lolote nuruni.
17 # Ay 18:11; 15:22; 18:5 Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao;
hujifanya rafiki na vitisho vya gizani.
18 # Ay 9:26; 22:16; Yud 1:23; Isa 57:20 “Lakini wao ni povu juu ya maji;
sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa,
hivyo hakuna hata mmoja
aendaye kwenye shamba la mizabibu.
19 # Ay 6:17; 21:13 Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka,
ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi.
20 # Ay 18:17; Mit 10:7; Dan 4:14; Za 31:12 Tumbo lililowazaa huwasahau,
nao huwa karamu ya mabuu;
watu waovu hawakumbukwi tena,
lakini huvunjika kama mti.
21 # Ay 22:9 Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto,
nao hawaonyeshi huruma kwa wajane.
22 # Kum 28:66; Mt 6:27 Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake;
ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha.
23 # Ay 9:24; Amo 6:1; 2Nya 16:9; Ay 10:4 Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama,
lakini macho yake yanaona njia zao.
24 # 2Fal 19:35; Za 37:35-36; 83:13; Isa 17:5 Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka;
hushushwa na kukusanywa kama wengine wote,
hukatwa kama masuke ya nafaka.
25 # Ay 16:17; 27:4 “Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo,
na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu