25
Bildadi Anasema: Mwanadamu Awezaje Kuwa Mwadilifu Mbele Za Mungu?
1 #
Ay 8:1
Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:
2 #
Zek 9:2; Ufu 1:6 “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;
yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.
3 #
Mt 5:45; Yak 1:17; Mwa 1:14-16 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?
Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?
4 #
Ay 4:17; 14:4; Rum 3:19-20 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?
Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?
5 #
Ay 31:26; 4:18 Ikiwa hata mwezi sio mwangavu
nazo nyota si safi machoni pake,
6 #
Za 22:6; 80:17; Eze 2:1; Ay 7:5 sembuse mtu ambaye ni funza:
mwanadamu ambaye ni buu tu!”