Ayubu 26
NMM

Ayubu 26

26
Hotuba Ya Tisa Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki
1Kisha Ayubu akajibu:
2 # Ay 6:12; 4:3; Za 71:9; Mit 25:11 “Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!
Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!
3 # Ay 34:35 Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?
Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!
4 # 1Fal 22:24 Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?
Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?
5 # Za 88:10; Isa 14:9 “Wafu wako katika maumivu makuu,
wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake.
6 # Za 139:8; Mit 15:11; Ebr 4:13; Amo 9:2 Mauti#26:6 Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol. iko wazi mbele za Mungu;
Uharibifu#26:6 Kwa Kiebrania ni Abadon. haukufunikwa.
7 # Ay 9:8 # Ay 8:22; 31:35 Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu;
naye huining’iniza dunia mahali pasipo na kitu.
8 # Mit 30:4; Za 147:8 Huyafungia maji kwenye mawingu yake,
hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
9 # 2Sam 22:10; Za 97:2 Huufunika uso wa mwezi mpevu,
akitandaza mawingu juu yake.
10 # Mit 8:27; Isa 40:22; Ay 28:3 Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji,
ameweka mpaka wa nuru na giza.
11 # 2Sam 22:8 Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,
zinatishika anapozikemea.
12 # Isa 51:15; Kut 14:21; Yer 31:35; Ay 12:13; Kut 14:21; Ay 12:13; 9:13 Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari;
kwa hekima yake alimkata Rahabu#26:12 Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. vipande vipande.
13 # Za 33:6; Isa 27:1 Aliisafisha anga kwa pumzi yake;
kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.
14 # Ay 9:6; 36:29 Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake;
tazama jinsi ulivyo mdogo mnong’ono tunaousikia kumhusu!
Ni nani basi awezaye kuelewa
ngurumo za nguvu zake?”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu