27
Hotuba Ya Mwisho Ya Ayubu
Ayubu Anadumisha Uadilifu Wake
1 #
Ay 29:1
Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
2 #
Ay 9:18; 34:5; Isa 45:9; 1Sam 1:10 “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu,
Mwenyezi ambaye amenifanya
nionje uchungu wa nafsi,
3 #
Mwa 2:7; Za 144:4 kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu,
nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,
4 #
Ay 6:28; 12:16; 16:17 midomo yangu haitanena uovu,
wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 #
Ay 2:9; 10:7; 32:2 Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi;
hadi nife, sitakana uadilifu wangu.
6 #
Ay 29:14; Za 119:121; Isa 59:17; 61:10; Rum 2:15 Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha;
dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.
7“Watesi wangu wawe kama waovu,
nao adui zangu wawe kama wasio haki!
8 #
Ay 8:13; Hes 16:22; Lk 12:20; Mt 16:26 Kwa maana mtu asiyemcha Mungu
analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali,
Mungu anapouondoa uhai wake?
9 #
Zek 7:13; Mik 3:4; 1Sam 8:18 Je, Mungu husikiliza kilio chake,
shida zimjiapo?
10 #
Ay 22:26
Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi?
Je, atamwita Mungu nyakati zote?
11 #
Ay 36:23; 27:13 “Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu;
njia za Mwenyezi sitazificha.
12Ninyi nyote mmeona hili wenyewe.
Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?
13 #
Ay 15:20; 16:19 “Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu,
urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:
14 #
Mao 2:22; Es 9:10; Hos 9:13; Ay 20:10; 2Fal 10:6-10 Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani,
fungu lao ni kuuawa kwa upanga;
wazao wake hawatakuwa kamwe
na chakula cha kuwatosha.
15 #
Za 78:64
Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao,
nao wajane wao hawatawaombolezea.
16 #
Zek 9:3
Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi,
na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
17 #
Mit 13:22; Mhu 2:26 yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa,
naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
18 #
Ay 8:14; Isa 1:8; 24:20; Mao 2:6 Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui,
kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
19 #
Ay 3:13; Hes 20:26 Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho;
afunguapo macho yake, yote yametoweka.
20 #
Ay 15:21; 20:8 Vitisho humjia kama mafuriko;
dhoruba humkumba ghafula usiku.
21 #
Ay 38:24; Yer 13:24; Ay 30:22; 7:10; Yer 22:22 Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka;
humzoa kutoka mahali pake.
22 #
Yer 13:14; Eze 5:11; Ay 11:20 Humvurumisha bila huruma,
huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.
23 #
Ay 7:10; 18:18 Upepo humpigia makofi kwa dharau,
na kumfukuza atoke mahali pake.