Ayubu 28
NMM

Ayubu 28

28
Mapumziko: Imani Inakopatikana
1 # Za 12:6; 66:10; Yer 9:7; Mal 3:3; Dan 11:35 “Kuna machimbo ya fedha,
na mahali dhahabu isafishwapo.
2 # Kum 8:9 Chuma hupatikana ardhini,
nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini.
3 # Mhu 7:25; 8:17; Mit 2:4 Mwanadamu hukomesha giza;
huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali,
kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini
katika giza jeusi sana.
4 # 2Sam 5:8 Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu,
mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu;
mbali na wanadamu huning’inia na kupembea kwa kamba.
5 # Mwa 1:29; Za 145:15 Ardhi, ambako chakula hutoka,
chini hugeuzwa kwa moto;
6 # Isa 54:11; Wim 5:14; Ay 22:24 yakuti samawi hutoka katika miamba yake,
nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.
7 # Ay 28:21 Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika,
wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.
8 # Ay 41:34; Isa 35:9 Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga,
wala simba azungukaye huko.
9 # Kum 8:15; Yn 2:6 Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana,
na kuiacha wazi mizizi ya milima.
10 # Mit 2:4; Ay 28:4 Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba;
macho yake huona hazina zake zote.
11 # Mwa 7:11; Isa 48:6; Yer 33:3 Hutafuta vyanzo vya mito
na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.
12 # Mit 1:20; Mhu 7:24 “Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?
Ufahamu unakaa wapi?
13 # Mit 3:15; Mt 13:44-46 Mwanadamu hatambui thamani yake;
haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.
14Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’;
bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’
15 # Mit 16:16; Mdo 8:20 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote,
wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.
16Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri,
kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.
17 # Za 119:72; Mit 8:10; Ay 28:15 Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo,
wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.
18Marijani na yaspi hazistahili kutajwa;
thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu.
19 # Mit 3:14-15; 8:10-19 Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo,
wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.
20“Ni wapi basi hekima itokako?
Ufahamu hukaa wapi?
21 # Ay 28:7 Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai,
imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.
22 # Ay 26:6 Uharibifu na Mauti husema,
‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’
23 # Mdo 15:18; Ay 22:22; Mit 8:22-31 Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima
na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,
24 # Isa 11:12; Yos 3:11; Ebr 4:13; Za 66:7 kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia
na huona kila kitu chini ya mbingu.
25 # Ay 38:8-11; Za 135:7 Alipofanyiza nguvu za upepo
na kuyapima maji,
26 # Ay 38:25-27; Isa 35:7; Yer 14:22 alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua
na njia kwa ajili ya umeme wa radi,
27ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake,
akaithibitisha na kuihakikisha.
28 # Kut 20:20; Kum 4:6 Naye Mungu akamwambia mwanadamu,
‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,
nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu