31
1 #
Kum 5:18; Mt 5:18 “Nimefanya agano na macho yangu
yasimtazame msichana kwa kumtamani.
2 #
Ay 16:19; 20:29 Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu,
urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu?
3 #
Ay 21:30; 34:22; Rum 2:9 Je, si uharibifu kwa watu waovu,
maangamizi kwa wale watendao mabaya?
4 #
2Nya 16:9; Mit 5:21; Yer 32:19; Dan 4:37 Je, yeye hazioni njia zangu
na kuihesabu kila hatua yangu?
5 #
Ay 15:31; Mik 2:11 “Kama nimeishi katika uongo
au mguu wangu umekimbilia udanganyifu,
6 #
Law 19:36; Ay 6:2 Mungu na anipime katika mizani za uaminifu,
naye atajua kwamba sina hatia:
7 #
Ay 9:30; Hes 15:39; Eze 6:9; Mt 5:29; Mhu 11:9 kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia,
kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu,
au kama mikono yangu imetiwa unajisi,
8 #
Law 26:16; Yn 4:37; Mik 6:15 basi wengine na wale nilichokipanda,
nayo yale yote niliyootesha na yang’olewe.
9 #
Kum 11:16; Yak 1:14 “Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke,
au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu,
10 #
Kum 28:30; Yer 8:16; Mit 14:31 basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine,
nao wanaume wengine walale naye.
11 #
Law 20:10; Yn 8:4-5 Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu,
naam, dhambi ya kuhukumiwa.
12 #
Ay 15:30; 26:6 Ni moto uwakao kwa Uharibifu;#31:12 Kwa Kiebrania ni Abadon (Ay 26:6; Mit 15:11).
ungekuwa umeng’oa mavuno yangu.
13 #
Kut 21:2-11; Law 25:39-46 “Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu,
walipokuwa na manung’uniko dhidi yangu,
14 #
Ay 33:5; Hos 9:7; Za 10:13, 15; Isa 10:3; Yer 5:31 nitafanya nini Mungu atakaponikabili?
Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?
15 #
Ay 10:3; Efe 6:9 Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu,
si ndiye aliwaumba?
Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote
ndani ya mama zetu?
16 #
Law 25:17; Ay 20:19; Yak 1:27 “Ikiwa nimewanyima maskini haja zao,
au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,
17 #
Ay 6:27; 29:12 kama nimekula chakula changu mwenyewe,
bila kuwashirikisha yatima;
18 #
Isa 51:18
lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya,
nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane:
19 #
Ay 22:6; 24:4; Isa 58:7 kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo,
au mtu mhitaji asiye na mavazi
20 #
Ay 29:13; Amu 6:37 ambaye wala moyo wake haukunibariki
kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu,
21 #
Ay 22:7-9; Yak 1:27 na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima,
nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani,
22 #
Hes 15:30; Za 10:15 basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu,
nao na uvunjike kutoka kiungio chake.
23 #
Ay 10:3; 13:11; Mwa 20:11 Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu,
nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo.
24 #
Ay 22:25; Mk 10:24; Lk 12:15 “Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu,
au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’
25 #
Mwa 12:16; Isa 10:14 kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu,
ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata,
26 #
Hes 11:20; Kum 4:19; Eze 8:16 kama nimelitazama jua katika kung’aa kwake
au mwezi ukienda kwa fahari yake,
27 #
Ay 24:15; Yak 1:14; Yer 8:2; 16:11 hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri,
au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu,
28 #
Mwa 38:24; Kum 17:2-7; Yos 24:23-27; Mit 30:9 basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa,
kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana.
29 #
Za 35:15; Mt 5:44; Mit 17:5; 24:17-18 “Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu,
au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia,
30lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi
kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake;
31kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema,
‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’
32 #
Amu 19:20; Mt 25:35; Ebr 13:2; 1Pet 4:9 Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani,
kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri;
33 #
Za 32:5; Mit 28:13; Mwa 3:8 kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo,
kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu,
34 #
Kut 23:2; Mit 29:25 kwa sababu ya kuogopa umati wa watu,
na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa,
nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango:
35(“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia!
Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu:
Mwenyezi na anijibu;
mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi.
36Hakika ningeyavaa begani mwangu,
ningeyavaa kama taji.
37 #
Ay 1:3; 21:28 Ningempa hesabu ya kila hatua yangu,
ningemwendea kama mwana wa mfalme.)
38 #
Mwa 4:10
“Kama nchi yangu inalia dhidi yangu,
na mifereji yake yote imelowana kwa machozi,
39 #
1Fal 21:19; Law 19:13; Yak 5:4 kama nimekula mazao yake bila malipo,
au kuvunja mioyo ya wapangaji wake,
40 #
Mwa 3:18; Mit 13:7 basi miiba na iote badala ya ngano,
na magugu badala ya shayiri.”
Mwisho wa maneno ya Ayubu.