Ayubu 32
NMM

Ayubu 32

32
Sehemu Ya Tatu: Mazungumzo Ya Elihu
(Ayubu 32–37)
Elihu Awakemea Rafiki Za Ayubu
1 # Ay 2:3; 10:7 Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe. 2#Mwa 22:21; Ay 13:19; 35:2Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu. 3#Ay 42:7; 32:12-13; 15:13Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu. 4#Law 19:32Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye. 5Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.
6 # Ay 15:10 Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema:
“Mimi ni mdogo kwa umri,
nanyi ni wazee;
ndiyo sababu niliogopa,
sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.
7 # 1Nya 29:15; 2Nya 10:6 Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme,
nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’
8 # Ay 27:3; 33:4; Mit 2:6; 1Fal 3:9 Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu,
pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.
9 # 1Kor 1:21-26 Sio wazee peke yao walio na hekima,
sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.
10 # Ay 33:1; 31:33; Za 34:11; Ay 5:27 “Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi;
mimi nami nitawaambia lile ninalojua.
11Nilingojea mlipokuwa mnaongea,
nilizisikiliza hoja zenu;
mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema,
12 # Ay 32:3 niliwasikiliza kwa makini.
Lakini hakuna hata mmoja wenu
aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa;
hakuna hata mmoja wenu
aliyeweza kujibu hoja zake.
13 # Mhu 9:11; Yer 9:23 Msiseme, ‘Tumepata hekima;
Mungu na amthibitishe kuwa mwongo,
wala si mwanadamu.’
14 # Ay 23:4 Lakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu,
nami sitamjibu kwa kutumia hoja zenu.
15 # Ay 32:1 “Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema;
maneno yamewaishia.
16Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya,
kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu?
17 # Ay 5:27; 33:3; 36:4 Mimi nami nitakuwa na la kusema;
mimi nami nitasema lile nilijualo.
18 # Mdo 4:20; 1Kor 9:16; 2Kor 5:14 Kwa kuwa nimejawa na maneno,
nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma;
19 # Yer 20:9; Amo 3:8; Mt 9:17 ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai,
kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.
20 # Ay 4:2; Yer 6:11 Ni lazima niseme ili niweze kutulia;
ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu.
21 # Law 19:15; 2Nya 19:7; Mt 22:16 Sitampendelea mtu yeyote,
wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote;
22 # Ay 4:17; 9:9; Za 12:2-4 kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza,
Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu