Ayubu 33
NMM

Ayubu 33

33
Elihu Anamkemea Ayubu
1 # Ay 32:10; 6:28; 13:6 “Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu;
zingatia kila kitu nitakachosema.
2Karibu nitafungua kinywa changu;
maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu.
3 # Ay 27:4; 36:4 Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu;
midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.
4 # Mwa 2:7; Ay 10:3; 27:3 Roho wa Mungu ameniumba;
pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.
5 # Ay 13:18 Unijibu basi, kama unaweza;
jiandae kunikabili mimi.
6 # Ay 9:32; 4:19 Mimi ni kama wewe mbele za Mungu;
mimi pia nimetolewa kwenye udongo.
7 # Ay 13:21; 2Kor 2:4 Huna sababu ya kuniogopa,
wala mkono wangu haupaswi kukulemea.
8“Lakini umesema nikiwa ninakusikia,
nami nilisikia maneno yenyewe:
9 # Ay 10:7; 9:30; 16:17 ‘Mimi ni safi na sina dhambi;
mimi ni safi na sina hatia.
10 # Ay 13:24 Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu,
naye ananiona kama adui yake.
11 # Ay 13:27; Mit 3:6; Isa 30:21 Ananifunga miguu kwa pingu,
tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’
12 # Mhu 7:20; Za 8:4; Isa 55:8-9 “Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa,
kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
13 # Ay 40:2; Isa 45:9 Kwa nini unamlalamikia
kwamba yeye hamjibu mwanadamu?
14 # Za 62:11; Mwa 30:2; Mt 27:19 Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja,
au wakati mwingine kwa njia nyingine,
ingawa mwanadamu anaweza asielewe.
15 # Mwa 30:2; Mt 27:19 Mungu husema na mwanadamu katika ndoto,
katika maono ya usiku,
wakati usingizi mzito uwaangukiapo
wanadamu wasinziapo vitandani mwao,
16 # Ay 36:10 anaweza akasemea masikioni mwao,
na kuwatia hofu kwa maonyo,
17 # Ay 36:10, 15; 6:4; Za 88:15-16 ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya
na kumwepusha na kiburi,
18 # Yn 2:6; Zek 9:11; Ay 15:22; Mt 26:52 kuiokoa nafsi yake na shimo,
uhai wake usiangamizwe kwa upanga.
19 # Kum 8:5; Za 6:2; Isa 38:13 Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,
kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,
20 # Za 102; 4; Za 107:18; Ay 3:24 kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula
nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri.
21 # Ay 2:5; 16:8 Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda,
nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika,
sasa inatokeza nje.
22 # Ay 38:17; Za 9:13; 88:3; 107:18; 116:3 Nafsi yake inakaribia kaburi,
nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.
23 # Ay 36:9-10; Mik 6:8; Gal 3:19; Ebr 8:6; 9:15; Ay 36:9-10; Mik 6:8 “Kama bado kuna malaika upande wake
kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu,
wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake,
24 # Isa 38:17 kumwonea huruma na kusema,
‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni;
nimepata ukombozi kwa ajili yake’:
25 # 2Fal 5:14 ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto;
hurudishwa upya kama siku za ujana wake.
26 # Mit 8:35; 2Fal 20:2-5; Lk 2:52; Ezr 3:13; Za 13:5 Humwomba Mungu, akapata kibali kwake,
huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha;
Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.
27 # Hes 22:34; 2Sam 12:13; Ezr 9:13; Yak 2:13; Lk 15:21 Ndipo huja mbele za watu na kusema,
‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki,
lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili.
28 # Kut 15:13; Za 34:22; 107:20; Ay 17:16; 22:20 Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni,
nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’
29 # Yer 10:23; Flp 2:13 “Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu;
mara mbili hata mara tatu,
30 # Za 49:19; Isa 53:11; Zek 9:11 ili aigeuze nafsi yake toka shimoni,
ili nuru ya uzima imwangazie.
31 # Yer 23:18; Ay 32:10 “Ayubu, zingatia, nisikilize mimi;
nyamaza, nami nitanena.
32 # Ay 6:29; 35:2 Kama unalo lolote la kusema, unijibu;
sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia.
33 # Mit 10:8, 10, 19; Za 34:11 Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi;
nyamaza, nami nitakufundisha hekima.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu