36
Elihu Atukuza Wema Wa Mungu
1Elihu akaendelea kusema:
2“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha
kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu.
3 #
Ay 4:17; 8:3 Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali,
nami nitamhesabia haki Muumba wangu.
4 #
Ay 6:28; 13:6; 37:5, 16, 23; 32:17 Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo;
mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.
5 #
Za 31:22; 69:33; Hes 23:19; Rum 11:29 “Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu;
ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.
6 #
Ay 8:22; 4:10 Hawaachi waovu waendelee kuishi,
bali huwapa walioteswa haki yao.
7 #
Za 34:15; 113:8; Mt 6:18; Isa 22:23 Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki;
huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme
na kuwatukuza milele.
8 #
2Sam 3:34; 2Fal 23:33 Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo,
wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,
9 #
Ay 15:25
huwaonyesha yale waliyoyatenda,
kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.
10 #
Ay 33:16; 2Fal 17:13; Ay 5:17 Huwafanya wao kusikia maonyo,
na huwaagiza kutubu uovu wao.
11 #
Kut 28:1; Hag 1:12; Isa 1; 19 Kama wakitii na kumtumikia,
wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio,
na miaka yao katika utoshelevu.
12 #
Law 26:38; Ay 15:22; 4:21; Efe 4:18 Lakini wasiposikiliza,
wataangamia kwa upanga,
nao watakufa pasipo maarifa.
13 #
Ay 15:12; Rum 2:5; Ay 5:2; 4:17; Amo 4:11 “Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki;
hata anapowafunga, hawamwombi msaada.
14 #
Kum 23:17
Wanakufa wangali vijana,
miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.
15 #
Ay 5:15; 2Kor 12:10; Ay 33:16; 34:33 Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao,
na kuzungumza nao katika dhiki zao.
16 #
Hos 2:14; Za 23:5; 78:19 “Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki,
ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi,
hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.
17 #
Ay 20:29; 22:11 Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu;
hukumu na haki vimekukamata.
18 #
Kut 23:8; Amo 5:12; Ay 34:33 Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri;
usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa.
19 #
Za 49:6; Yer 9:23 Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi
vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki?
20 #
Ay 34:20-25
Usiutamani usiku uje,
ili uwaburute watu mbali na nyumba zao.
21 #
Ay 34:33; Za 66:18; Ebr 11:25 Jihadhari usigeukie uovu,
ambao unaupenda zaidi kuliko mateso.
22 #
Isa 40:13; Rum 11:34 “Mungu ametukuzwa katika nguvu zake.
Ni nani aliye mwalimu kama yeye?
23 #
Ay 34:10, 13; Rum 11:33; Mwa 18:25; Kum 32:4 Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake,
au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?
24 #
1Nya 16:24; Za 35:27; 59:16; Ufu 15:3 Kumbuka kuzitukuza kazi zake,
ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
25 #
Rum 1:20
Wanadamu wote wameiona;
watu wanaikazia macho kwa mbali.
26 #
1Kor 13:12; Mwa 21:33; Ebr 1:12 Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu,
kupita ufahamu wetu!
Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27 #
2Sam 1:21; Za 147:8 “Yeye huvuta juu matone ya maji,
ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;
28 #
Ay 22:11; Mt 5:45 mawingu huangusha chini maji yake,
nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.
29 #
Mit 8:28; Isa 40:22 Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu,
jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.
30 #
Kut 19:16; Yer 10:13; Hab 3:11; Isa 51:10; Za 18:12, 14; 97:4 Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka,
naye huvifunika vilindi vya bahari.
31 #
1Fal 17:1; Amo 4:7-8; Isa 30:23; Mdo 14:17 Hivi ndivyo atawalavyo mataifa,
na kuwapa chakula kwa wingi.
32 #
Ay 28:24; Za 18:14 Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi,
na kuuagiza kulenga shabaha yake.
33Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja;
hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.#36:33 Au: hutangaza kuja kwake.