38
Sehemu Ya Nne: Mungu Anazungumza
(Ayubu 38–41)
Bwana Anamjibu Ayubu
1 #
1Sam 2:10; Eze 1:4; Kut 19:16-18; Ay 11:5; 40:6; Isa 21:1 Kisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:
2 #
Mk 10:38; 1Tim 1:7 “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza
kwa maneno yasiyo na maarifa?
3 #
Ay 40:7; 42:4; Mk 11:29; 1Fal 18:46 Jikaze kama mwanaume;
nitakuuliza swali,
nawe unijibu.
4 #
Mwa 1:1; Mit 8:29; Za 104:5 “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?
Niambie, kama unafahamu.
5 #
Za 102:25; Yer 31:37 Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake?
Hakika wewe unajua!
Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?
6 #
Mit 8:25; Ay 26:7 Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini,
au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,
7 #
Mwa 1:16; Za 19:1-4; 148:2-3; 1Fal 22:19; Kum 16:15 wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,
na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?
8 #
Za 33:7; Yer 5:22; Mwa 1:9-10 “Ni nani aliyeifungia bahari milango
ilipopasuka kutoka tumbo,
9 #
Mwa 1:2
nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,
na kuyafungia katika giza nene,
10 #
Za 33:7; Neh 3:3; Isa 40:12; Ay 7:12 nilipoamuru mipaka yake,
na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,
11 #
Za 65:7; 89:9; 104:6-9 niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi;
hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?
12 #
Za 57:8; 74:16; Amo 5:8 “Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,
au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,
13yapate kushika miisho ya dunia,
na kuwakung’uta waovu waliomo?
14 #
Kut 28:11
Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri;
sura yake hukaa kama ile ya vazi.
15 #
Kum 28:29; Ay 15:22; Mwa 17:14; Za 10:15 Waovu huzuiliwa nuru yao,
nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.
16 #
Mwa 1:7; Ay 9:8 “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?
Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?
17 #
Za 9:13; Mt 16:18 Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti?
Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti?
18 #
Ay 28:24; Isa 40:12; Ay 38:4 Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia?
Niambie kama unajua haya yote.
19 #
Mwa 1:4; Ay 28:3; Za 139:11-12 “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi?
Nako maskani mwa giza ni wapi?
20 #
Ay 24:13
Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake?
Unajua njia za kufika maskani mwake?
21 #
Ay 15:7
Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa!
Kwani umeishi miaka mingi!
22 #
Ay 37:6; Kum 28:12; Za 105:32; 147:17 “Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji,
au kuona ghala za mvua ya mawe,
23 #
Za 27:5; Isa 28:17; Eze 13:13; Ufu 16:21; Kut 9:18; Za 9:13 ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu,
na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano?
24 #
Ay 28:24; 27:21; Yer 10:13; 51:16 Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa,
au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia?
25 #
Ay 28:26
Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi
na njia ya umeme wa radi,
26 #
Ay 36:27; Za 84:6; 107:35; Isa 41:18 ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu,
jangwa lisilo na yeyote ndani yake,
27 #
Ay 28:26; 37:13; Za 104:14 ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa,
na majani yaanze kumea ndani yake?
28 #
2Sam 1:21; Yer 14:22 Je, mvua ina baba?
Ni nani baba azaaye matone ya umande?
29 #
Za 147:16-17
Barafu inatoka tumbo la nani?
Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni,
30 #
Ay 37:10
wakati maji yawapo magumu kama jiwe,
wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda?
31 #
Ay 9:9; Amo 5:8 “Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia?
Waweza kulegeza kamba za Orioni?
32 #
2Fal 23:5; Isa 13:10; 40:26; 45:12; Yer 19:13; Mwa 1:16 Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake,
au kuongoza Dubu na watoto wake?
33 #
Za 148:6; Yer 31:38 Je, unajua sheria zinazotawala mbingu?
Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?
34 #
Ay 5:10; 22:11 “Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni,
na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji?
35 #
Ay 36:32
Je, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake?
Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’?
36 #
Ay 34:32; Yak 1:5; Za 51:6; Mhu 2:26 Ni nani aliyeujalia moyo hekima
au kuzipa akili ufahamu?
37 #
Yos 3:16; Ay 22:11 Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu?
Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni
38 #
Law 26:19
wakati mavumbi yawapo magumu,
na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?
39 #
Mwa 49:9; Za 104:21 “Je, utamwindia simba jike mawindo,
na kuwashibisha simba wenye njaa
40 #
Ay 37:8; Mwa 49:9 wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao,
au wakivizia kichakani?
41 #
Mwa 8:7; Lk 12:24; Za 147:9; Mt 6:26 Ni nani ampaye kunguru chakula
wakati makinda yake yanamlilia Mungu,
yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?