4
Elifazi Anazungumza: Ayubu Ametenda Dhambi
1 #
Mwa 36:11; Ay 15:1; 22:1 Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:
2 #
Yer 4:19; 20:9; Ay 32:20 “Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe,
kutakukasirisha?
Lakini ni nani awezaye
kujizuia asiseme?
3 #
Sef 3:16; Hos 6:3; Ebr 12:12; Kum 32:2; Ay 29:23; 26:2; Za 71:9; Isa 13:7; 35:3 Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi,
jinsi ambavyo umeitia nguvu
mikono iliyokuwa dhaifu.
4 #
Yer 31:8; Ay 16:5; 29:16, 25; Isa 1:17; Isa 35:3; Ebr 12:12 Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa;
umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.
5 #
Rut 1:13; Za 38:2; Ay 6:14; Mit 24:10; Lk 4:23 Lakini sasa hii taabu imekujia wewe,
nawe unashuka moyo;
imekupiga wewe,
nawe unafadhaika.
6 #
Mwa 6:9; Za 71:5; Mit 3:26; Ay 1:1; 1Fal 18:19 Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa
ndiyo matumaini yako
na njia zako kutokuwa na lawama
ndilo taraja lako?
7 #
Za 41:12; 91:9-10; 37:25; 2Pet 2:9; Mit 12:21; Ay 5:11; 36:7; Mt 19:23 “Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia?
Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa?
8 #
Amu 14:18; Gal 6:7-8; Hos 8:7; Za 7:14; Yos 1:9; Ay 5:3; 15:17; Ay 5:6; 15:35; Mt 11:18 Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza,
wale walimao ubaya
na wale hupanda uovu,
huvuna hayo hayo hayo.
9 #
Kut 15:10; 2The 2:8; Law 26:38; Isa 25:7; Ay 41:21; 40:13 Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa;
kwa mshindo wa hasira zake huangamia.
10 #
Ay 38:15; 29:17; Za 22:13; 17:12; 22:21; Mt 28:15 Simba anaweza kunguruma na kukoroma,
lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika.
11 #
Kum 28:41; Mit 30:14; Ay 5:4; Za 34:10; 58:6; Ay 27:14; 29:17 Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo,
nao wana wa simba jike hutawanyika.
12 #
Ay 26:14; 33:14; 32:13; 12:23; Yer 9:23; Za 78:59 “Neno lililetwa kwangu kwa siri,
masikio yangu yakasikia mnong’ono wake.
13 #
Ay 33:15
Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku,
hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu,
14 #
Dan 10:8; Hab 3:16; Ay 21:6; Za 48:6; 55:5; 119:120, 161; Yer 5:22; 2Kor 7:15 hofu na kutetemeka kulinishika
na kufanya mifupa yangu yote itetemeke.
15 #
Za 104:4; Mt 14:26; Ebr 1:14; Dan 5:6; 7:15, 28; 10:8 Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu,
nazo nywele za mwili wangu zikasimama.
16 #
1Fal 19:12
Yule roho akasimama,
lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani.
Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu,
kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti:
17 #
Za 143:2; Mdo 17:24; Mal 2:10; Mit 20:9; Ay 9:2; 8:3; 10:3; 14:4; 15:14; 13:18; Mhu 7:20; Isa 51:13 ‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu?
Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?
18 #
Ay 25:5; 21:22; 5:4; 1Pet 2:4; Ebr 1:14 Kama Mungu hawaamini watumishi wake,
kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,
19 #
Isa 64:8; 2Kor 4:7; 2Pet 2:4; Mwa 2:7 ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba
za udongo wa mfinyanzi,
ambazo misingi yake ipo mavumbini,
ambao wamepondwa kama nondo!
20 #
Za 89:47; 90:5-6; Yak 4:14; Ay 14:2, 20; 15:33; 20:7 Kati ya mawio na machweo
huvunjwa vipande vipande;
bila yeyote kutambua,
huangamia milele.
21 #
Ay 8:22; Isa 38:12; Mit 5:23; Yn 8:24; Yer 9:3 Je, kamba za hema yao hazikung’olewa,
hivyo hufa bila hekima?’