40
1 #
Ay 5:8; 13:3; Ay 13:3; 9:15; 9:3; 11:8; 33:13 Bwana akamwambia Ayubu:
2 #
Rum 9:20
“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha?
Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”
3Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
4 #
Ay 42:6; Amu 18:19; Ay 29:9; Ezr 9:6; Zek 2:13 “Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe?
Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.
5 #
Ay 9:3; 9:15 Nimesema mara moja, lakini sina jibu;
naam, nimesema mara mbili,
lakini sitasema tena.”
6 #
Kut 14:21; Ay 38:1 Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:
7 #
Ay 38:3
“Jikaze kama mwanaume;
nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.
8 #
Ay 15:25; Rum 3:3; Za 51:4 “Je, utabatilisha hukumu yangu?
Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?
9 #
2Nya 32:8; Za 98:1; Kut 20:19; Za 29:3-4 Je, una mkono kama wa Mungu,
nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?
10 #
Za 29:1-2; 45:3; 93:1; 96:6; 104:1; 145:5 Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari,
nawe uvae heshima na enzi.
11 #
Nah 1:6; Sef 1:18; Za 18:27; Isa 32:19 Fungulia ukali wa ghadhabu yako,
mtafute kila mwenye kiburi umshushe,
12 #
Za 52:5; 1Pet 5:5; Dan 5:20; Mal 4:3; Lk 18:14 mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze,
waponde waovu mahali wasimamapo.
13 #
Hes 16:31-34; Ay 4:9 Wazike wote mavumbini pamoja;
wafunge nyuso zao kaburini.
14 #
Kut 15:6; Isa 63:5 Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia
kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.
15 #
Ay 9:9; Isa 11:7; 65:25 “Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,#40:15 Huyu alikuwa mnyama wa nyakati za zamani ambaye hajulikani hasa ni gani.
niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe,
anayekula majani kama ng’ombe.
16 #
Ay 39:11; 41:9 Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake,
uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!
17 #
Ay 41:15
Mkia wake hutikisika kama mwerezi;
mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.
18 #
Ay 41:12; Isa 11:4; 49:2 Mifupa yake ni bomba za shaba,
maungo yake ni kama fito za chuma.
19 #
Za 40:5; Isa 27:1 Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu,
lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.
20 #
Za 104:14, 26 Vilima humletea yeye mazao yake,
nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.
21 #
Mwa 41:2; Za 68:30; Isa 35:7; Ay 8:11 Hulala chini ya mimea ya yungiyungi,
katika maficho ya matete kwenye matope.
22 #
Za 1:3; Isa 44:4 Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake;
miti mirefu karibu na kijito humzunguka.
23Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu;
yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.
24 #
2Fal 19:28; Isa 37:29 Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho,
au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?