Ayubu 5
NMM

Ayubu 5

5
Elifazi Anaendelea
1 # Ay 15:15; Za 89:5-7; Hab 1:2 “Ita kama unataka, lakini ni nani atakayekujibu?
Ni yupi kati ya hao watakatifu utakayemgeukia?
2 # Mit 12:16; Gal 5:26; Ay 21:15; 36:13 Kuweka uchungu moyoni humuua mpumbavu,
nao wivu humchinja mjinga.
3 # Isa 40:24; Eze 17:6; Za 109:9-10; 37:35; 37:22; Mit 3:33; Ay 4:8; 24:18; Yer 12:2; Mit 6:15 Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akistawi,
lakini ghafula nyumba yake ikawa imelaaniwa.
4 # Ay 20:10; 4:11, 19; Amo 5:12; Za 109:12; Isa 9:17; 1Yn 2:1 Watoto wake wako mbali na usalama,
hushindwa mahakamani bila mtetezi.
5 # Law 26:16; Mik 6:15; Amu 2:15; Ay 20:18; 31:8 Wenye njaa huyala mavuno yake,
wakiyatoa hata katikati ya miiba,
nao wenye kiu huitamani sana mali yake.
6 # Ay 4:8 Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo,
wala udhia hauchipui kutoka ardhini.
7 # Mwa 3:17; Mit 22:8; Ay 10:17; 15:35; Za 51:5; 58:3; 90:10 Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika,
kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu.
8 # Za 50:15; 27:14; 35:23; Ay 8:5; 11:13; 13:3, 15; 13:4; 40:1; Yer 12:1; 1Kor 4:1 “Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu,
ningeliweka shauri langu mbele zake.
9 # Za 78:4; 11:2; Kum 29:9; Ay 9:4, 10; 11:7; 25:2; 26:14; Isa 40:28; Rum 11:23 Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa,
miujiza isiyoweza kuhesabika.
10 # Za 135:7; Yer 14:22; Mt 5:45; Law 26:4; Ay 36:28; 37:6, 13 Yeye huipa nchi mvua,
huyapeleka maji kunyesha mashamba.
11 # 1Sam 2:7-8; Ay 4:7; Za 75:7; 113:7-8; Isa 61:2; Rum 12:5; Yak 4:10; Mt 23:12; 5:4 Huwainua juu wanyonge,
nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama.
12 # Isa 8:10; Yer 19:7; Neh 4:15; Isa 19:3; Za 33:10; 78:59; Ay 12:23 Huipinga mipango ya wenye hila,
ili mikono yao isifikie ufanisi.
13 # Za 36:3; Lk 20:23; Ay 37:24; Isa 29:14; 44:25; Yer 8:8; 18:18; 51:57; 1Kor 3:19; 2Kor 11:3 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao,
nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali.
14 # Isa 8:22; Yn 12:35; Amo 8:9; Ay 15:22, 30; 18:6; Kum 28:29 Giza huwapata wakati wa mchana;
wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku.
15 # Kut 22:23; Ay 4:10; 8:6; 22:27; 33:26; 36:15; 35:10 Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao;
huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu.
16 # Za 63:11; Rum 3:19; Ay 20:19; 31:16; Mit 17:5; 22:22; Isa 11:4; 41:17; 61:1 Kwa hiyo maskini analo tarajio,
nao udhalimu hufumba kinywa chake.
17 # Sef 3:7; Yak 1:12; Mit 3:11; Yer 31:18; Ebr 12:5-11; Za 94:12; Yak 1:12; Kum 8:5; Ay 33:19; 36:10; Ebr 12:5-11 “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi;
kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.#5:17 Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania Shaddai (hapa na kila mahali katika kitabu hiki cha Ayubu).
18 # Isa 30:26; Kum 32:39; 1Sam 2:6; Isa 57:15; 61:1; Hos 6:1 Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga;
huumiza, lakini mikono yake pia huponya.
19 # Mit 3:25-26; Kut 12:46; Za 34:19; 91:10; Mit 1:33; 2The 3:3; 2Pet 2:9 Kutoka majanga sita atakuokoa;
naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe.
20 # Ay 5:22; Za 33:19; 22:20; 91:7; 140:7; 144:10; Yer 39:18 Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo,
naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.
21 # Za 31:15; 12:2-4; 31:20; 23:4; 27:1; 91:5; Ay 5:15 Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi,
wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia.
22 # Hos 2:18; Mk 1:14; Ay 8:21; 39:7, 18, 22; 41:29; 5:20; Law 25:18; Za 91:13 Utayacheka maangamizo na njaa,
wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa
wanyama wakali wa mwituni.
23 # 2Fal 3:19-25; Mt 13:8; Isa 65:25; Eze 34:25; Za 91:12; Isa 28:15; Hos 2:18; Za 91:12 Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba,
nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe.
24 # Ay 12:6; 21:9; 8:6; 22:23 Utajua ya kwamba hema lako li salama;
utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua.
25 # Kum 28:4; Za 72:16; Isa 48:19; 44:3-4 Utajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi,
nao wazao wako wengi kama majani ya nchi.
26 # Kum 11:21; Mhu 8:13; Mwa 15:15; Mit 3:21-26 Utaingia kaburini ukiwa na umri wa uzee mtimilifu,
kama masuke ya ngano yakusanywapo kwa wakati wake.
27 # Ay 32:10; 8:5; 11:13; 22:27 “Tumelichunguza hili, nalo ni kweli.
Hivyo lisikie na ulitendee kazi.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu