Ayubu 6
NMM

Ayubu 6

6
Hotuba Ya Pili Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Malalamiko Yangu Ni Ya Haki
1Kisha Ayubu akajibu:
2 # Ay 31:6; Mit 11:1; Dan 5:27 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa,
nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani!
3 # Mit 27:3; Ay 21:4; 16:6; 2Fal 4:29; Ay 6:11, 26; 7:11; 16:6 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote,
kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka.
4 # Kum 32:23; Za 38:2; 88:15-18; Mao 3:12; Ay 16:12-14; Za 7:13; 18:14; 21:12; Mwa 17:1; Ay 7:20; 6:12, 13; Kum 32:32 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu,
roho yangu inakunywa sumu yake;
vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.
5 # Mwa 16:12; Ay 30:7; 30:24 Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani,
au ng’ombe dume hulia akiwa na chakula?
6 # Ay 33:20; Za 107:18 Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi,
au upo utamu katika ute mweupe wa yai?
7 # Za 31:22 Ninakataa kuvigusa;
vyakula vya aina hii hunichukiza.
8“Laiti ningepata haja yangu,
kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,
9 # 1Fal 19:4; Za 31:22 kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda,
kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali!
10 # Mk 8:38; Za 119:102; Law 19:2; 2Fal 19:22; Ay 2:11; 15:11; Za 94:19; 38:17; Yer 4:19; 45:3; Ay 22:22; 23:12 Ndipo bado ningekuwa na hii faraja,
furaha yangu katika maumivu makali:
kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu.
11 # Ay 6:3 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini?
Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu?
12 # Ay 26:2 Je, mimi nina nguvu za jiwe?
Je, mwili wangu ni shaba?
13 # Ay 26:2 Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe,
wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami?
14 # Ay 4:5; 15:4; 1Sam 20:42; Za 38:11; 69:20; 1Yn 3:17; Mwa 17:1 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,
hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.
15 # Ay 13:4; 16:2; 21:34; Za 22:1; 38:11; Yer 15:18 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,
ni kama vijito vya msimu,
ni kama vijito ambavyo hufurika
16 # Za 147:18 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,
ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,
17 # Ay 24:19 lakini hukauka majira ya ukame,
na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.
18Misafara hugeuka kutoka njia zake;
hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia.
19 # Mwa 25:15; Isa 21:14; Mwa 10:7, 28 Misafara ya Tema inatafuta maji,
wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri
hutazama kwa matarajio.
20 # Yer 14:3; Yoe 1:11 Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini;
wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia.
21 # Za 38:11 Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote;
mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa.
22 # Mdo 20:33; Hes 35:31; Ay 33:24; Za 49:7; Yer 15:10 Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu,
au mnilipie fidia kutoka mali zenu,
23 # 2Fal 19:19 au niokoeni mikononi mwa adui,
au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’?
24 # Mit 17:27; Mhu 5:2; Ay 2:10; 33:33; Za 39:1; 141:3; 39:1; Mit 10:19 “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya;
nionyesheni nilikokosea.
25 # Mhu 12:11; Isa 22:23 Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli!
Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini?
26 # Mwa 41:6; Yer 5:13; Ay 6:3; 8:2; 15:3; 16:3 Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema,
na kuyafanya maneno ya mtu anayekata tamaa kama upepo?
27 # Nah 3:10; 2Pet 2:3; Eze 24:6; Yoe 3:3; Oba 1:11; Kut 22:22, 24; Isa 10:2; Ay 31:17 Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima,
na kubadilishana rafiki yenu na mali.
28 # Ay 9:15; 24:25; 27:4; 34:10; 33:1, 3; 34:6; 36:3, 4 “Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi.
Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu?
29 # Za 66:10; Zek 13:9; Ay 19:6; 27:2; 40:8; Isa 40:27; Ay 2:3; 9:21; 10:7 Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu;
angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu.#6:29 Au: haki yangu bado inasimama.
30 # Ay 27:4; 33:8-12; Yak 3:13; Ay 12:11 Je, pana uovu wowote midomoni mwangu?
Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila?

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu