Ayubu 8
NMM

Ayubu 8

8
Bildadi Anasema: Yampasa Ayubu Atubu
1 # Mwa 25:2; Ay 18:1; 25:1 Kisha Bildadi Mshuhi akajibu:
2 # Ay 6:26; 11:2; 2Nya 36:16 “Hata lini wewe utasema mambo kama haya?
Maneno yako ni kama upepo mkuu.
3 # Mwa 18:25; 2Nya 19:7; Kum 32:4; Ay 34:12; Dan 9:14 Je, Mungu hupotosha hukumu?
Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?
4 # Ay 1:5, 18 Watoto wako walipomtenda dhambi,
aliwapa adhabu ya dhambi yao.
5 # Ay 5:8; 11:13; 22:23 Lakini ukimtafuta Mungu,
nawe ukamsihi Mwenyezi,
6 # Za 7:6; Isa 58:9; Ay 5:24; 5:15; 22:27; Isa 65:24 ikiwa wewe ni safi na mnyofu,
hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako,
na kukurudisha katika mahali pako pa haki.
7 # Ay 21:13; 22:21; 36:11; Za 25:13; Yer 29:11; 31:17 Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo,
lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.
8 # Kum 4:32; 32:7; Za 71:18; Ay 15:18 “Ukaulize vizazi vilivyotangulia
na uone baba zao walijifunza nini,
9 # Mwa 47:9; 2Nya 10:6; Za 39:5-6; 1Nya 29:15; Ay 7:6 kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote,
nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.
10 # Mt 1:8; 2:1-2; 4:1 Je, hawatakufundisha na kukueleza?
Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?
11 # Ay 40:21; Kut 2:3; Isa 19:6; 35:7 Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope?
Matete yaweza kustawi bila maji?
12 # Isa 34:4; Yer 17:6; Za 129:6; Yak 1:10, 11; 1Pet 1:24 Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa,
hunyauka haraka kuliko majani mengine.
13 # Za 50:13; 112:10; Mit 10:28; Yer 15:9; Ay 11:20; 18:14; Isa 33:14; Mt 24:51; Lk 12:1 Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu;
vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.
14 # Ay 8:15; 27:18; Isa 59:5 Lile analolitumainia huvunjika upesi;
lile analolitegemea ni utando wa buibui.
15 # Ay 27:18; 8:12; Za 49:11; Mt 7:26-27 Huutegemea utando wake, lakini hausimami;
huung’ang’ania, lakini haudumu.
16 # Za 80:11; 37:35; Isa 16:5; Yer 11:16 Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua,
ukieneza machipukizi yake bustanini;
17huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe,
na kutafuta nafasi katikati ya mawe.
18 # Ay 14:20; 7:10; Za 37:36; 103:16 Unapong’olewa kutoka mahali pake,
ndipo mahali pale huukana na kusema,
‘Mimi kamwe sikukuona.’
19 # Za 113:7 Hakika uhai wake hunyauka,
na kutoka udongoni mimea mingine huota.
20 # Mwa 18:25; Ay 21:30; 1The 5:23-24; Za 37:24 “Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia,
wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya.
21 # Ay 5:22; Ezr 3:13; Isa 35:6; Za 47:5; 107:22 Bado atakijaza kinywa chako na kicheko,
na midomo yako na kelele za shangwe.
22 # Za 6:10; Eze 7:27; 1Sam 8:3; Mit 14:11; Ay 18:6 Adui zako watavikwa aibu,
nazo hema za waovu hazitakuwepo tena.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu