9
Hotuba Ya Tatu Ya Ayubu
Hakuna Mpatanishi
1Kisha Ayubu akajibu:
2 #
Za 143:2; Rum 3:20; Ay 4:17 “Naam, najua hili ni kweli.
Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?
3 #
Ay 9:32; 40:5; Za 44:21 Ingawa mtu angetaka kushindana naye,
asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.
4 #
Mit 2:6; 8:6; Mhu 2:26; 2Nya 13:12; Isa 40:26; Ay 5:9; 12:13; Za 93:4; Dan 2:20 Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno.
Ni nani aliyempinga naye akawa salama?
5 #
Isa 13:13; Mik 1:4; Mt 17:20; Za 18:7 Aiondoa milima bila yenyewe kujua
na kuipindua kwa hasira yake.
6 #
Hag 2:6; 2:21; Ebr 12:26; Isa 2:19-21; 2Sam 22:8 Aitikisa dunia kutoka mahali pake
na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.
7 #
Yer 4:23; Eze 32:8; Isa 34:4; Sef 1:15; Yoe 2:2 Husema na jua, nalo likaacha kuangaza;
naye huizima mianga ya nyota.
8 #
Mwa 1:1, 8; Isa 48:13; Ay 38:16; Za 77:19; Mit 8:28; Hab 3:15 Yeye peke yake huzitandaza mbingu
na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9 #
Mwa 1:16; Ay 38:31; 32:22; Amo 5:8 Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu,#9:9 Nyota za Dubu hapa ina maana ya kundi la nyota za kaskazini, ambazo zinaitwa kwa jina la Dubu Mkuu. na Orioni,#9:9 Orioni ni kundi la nyota kubwa.
Kilimia,#9:9 Kilimia ni jina lililopewa nyota saba (Taurus). na makundi ya nyota za kusini.
10 #
Kum 6:22; Za 72:18; 136:4; Yer 32:20 Hutenda maajabu yasiyopimika,
miujiza isiyoweza kuhesabiwa.
11 #
Ay 23:8-9; 35:14 Anapopita karibu nami, siwezi kumwona;
apitapo mbele yangu, simtambui.
12 #
Hes 23:20; Isa 43:13; 14:27; Dan 2:21; Rum 9:20; Ay 11:10 Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia?
Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’
13 #
Hes 14:18; Ay 10:15; Za 78:38; Isa 3:11; 6:5 Mungu hataizuia hasira yake;
hata jeshi kubwa la Rahabu#9:13 Rahabu hapa ina maana ya Misri kwa fumbo. lenye nguvu
linajikunyata miguuni pake.
14 #
Ay 9:3
“Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye?
Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye?
15 #
Ay 10:15; 13:19; 34:5-6; 40:5; 42:7; Mwa 18:25; 1Sam 24:12; Za 50:6; 96:13 Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu;
ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.
16 #
Ay 13:22; Rum 9:20-21 Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali,
siamini kama angenisikiliza.
17 #
Isa 38:13; 38:13; Yn 1:4; Za 10:10; 83:15; Ay 16:12; 30:16; 16:14; 2:3 Yeye angeniangamiza kwa dhoruba
na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.
18 #
Ay 7:19; 10:1 Asingeniacha nipumue
bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.
19 #
Ay 9:4; Neh 9:32; Yer 49:19 Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu!
Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?
20 #
Ay 9:15
Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu;
kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.
21 #
Mwa 6:9; Hes 11:15; Ay 7:15-16; 6:29; 10:1 “Ingawa mimi sina kosa,
haileti tofauti katika nafsi yangu;
nauchukia uhai wangu.
22 #
Mhu 9:2-3; Eze 21:3; Ay 3:19 Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema,
‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’
23 #
Hab 1:3; 1Pet 1:7; Ebr 11:36; Za 64:4 Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula,
yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa.
24 #
Za 73:3; 73:12; Mhu 8:11; Mao 3:9; Ay 1:15, 17; 10:3; 40:8; Yer 12:1; Isa 41:20 Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu,
yeye huwafunga macho mahakimu wake.
Kama si yeye, basi ni nani?
25 #
Ay 7:6, 7; 10:20 “Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji;
zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo.
26 #
Isa 18:2; Ay 39:29; Za 46:3; Hab 1:8 Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo,
mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.
27 #
Ay 7:11
Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu,
nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’
28 #
Kut 20:7; 34:7; Ay 3:25; 7:21 bado ninahofia mateso yangu yote,
kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.
29 #
Ay 9:3, 15; Za 37:33 Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia,
kwa nini basi nitaabishwe bure?
30 #
Hos 13:12; Isa 1:15-18; Mal 3:2; Ay 31:7; 14:4, 17; 17:9; Yer 2:22 Hata kama ningejiosha kwa sabuni
na kutakasa mikono yangu kwa magadi,
31 #
Za 35:7; 40:2; 51:9; Yer 2:22; Nah 3:6; Mal 2:3; Ay 7:20 wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi
kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.
32 #
Rum 9:20; Mhu 6:10; Za 143:2; Hes 23:19 “Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu,
ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.
33 #
1Sam 2:25; Ay 9:19 Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu,
aweke mkono wake juu yetu sote wawili,
34 #
Ay 6:4; 21:9; Za 39:10; 73:5; 32:4 mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu,
ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.
35 #
Ay 7:15; 13:21; 7:11 Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa,
lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.