Utangulizi
Shairi hili ndefu linahusu mojawapo ya matatizo ya ndani zaidi ya mwanadamu. Tunawezaje kuelezea hali ya dhambi na mateso, kama yupo Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wa kufanya jambo kuhusu mambo haya? Kitabu hiki kinaanza na mateso. Ayubu anapewa mseto wa hotuba tatu na baadhi ya marafiki zake: Elifazi, Bildadi, na Sofari. Kila mmoja anajaribu kuelezea majaribu ya Ayubu kwa njia tofauti. Elihu, mtu wa nne, anajaribu kueleza kwa kifupi hali hio kwa kutoa maelezo kwa nini Ayubu anataabika. Mwishowe Mwenyezi Mungu mwenyewe ananena na Ayubu. Ayubu anagundua kwamba hatuhitaji sana “majibu” ya matatizo yetu maishani, bali tunamhitaji Mwenyezi Mungu mwenyewe. Ayubu anaponywa na kupewa baraka za kiroho na za kimwili zilizokuwa zaidi ya hali yake ya hapo mwanzo.
Wazo Kuu
Fumbo linalozunguka maisha ya mwanadamu na hitaji la kumwamini Mwenyezi Mungu vinaenea katika kitabu hiki chote. Binadamu hana ujuzi wa kutosha kuelezea kwa nini mambo yanafanyika kwa njia fulani. Inawezekana kushinda vikwazo maishani kwa imani katika Mwenyezi Mungu, ingawa Mungu kweli anafahamu kwa nini mambo yote hutendeka, na kwamba wakati hatuna chochote kilichobaki ila Mwenyezi Mungu pekee, yeye Mungu anatosha.
Mwandishi
Hajulikani.
Tarehe
Karne ya 10 K.K.
Mgawanyo
• Kuanza kwa mateso za Ayubu (1:1–2:13)
• Hotuba za kwanza (3:1–14:22)
• Hotuba za pili (15:1–21:34)
• Hotuba za tatu (22:1–31:40)
• Hotuba ya Elihu (32:1–37:24)
• Mungu anamjibu Ayubu (38:1–41:34)
• Kurejezwa kwa Ayubu (42:1-17).