Yoeli Utangulizi
NMM

Yoeli Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kilichoandikwa kwa njia ya kupendeza kinatumia tauni ya nzige kama ishara ya kueleza hukumu ya Mwenyezi Mungu inayokuja juu ya Yerusalemu. Kama vile nzige waliharibu nchi, ndivyo nchi itakavyoharibiwa na majeshi ya adui kama taifa halingetubu dhambi zake. Kama watu wangeitikia mwito wa kutubu, kutakuwa na wakati wa ufanisi na kurudi kwa neema ya Mwenyezi Mungu. Neema ya Mwenyezi Mungu inaonekana kwenda zaidi ya siku zijazo hivi karibuni, hadi wakati ambao Mwenyezi Mungu atamimina Roho Mtakatifu kwa watu wote (2:28-32). Haya yanaonekana yakitimizwa katika Injili wakati wa Pentekoste (Matendo 2:16-21).
Wazo Kuu
Ujumbe wa Yoeli ni kuhusu hukumu ijayo kama watu wa Yerusalemu hawatatubu. Hakika kama vile nzige waliharibu na kuacha miti bila chochote, ndivyo Mwenyezi Mungu ataharibu na kuacha nchi bila chochote. Yoeli anaongea kuhusu ufanisi unaokuja na baraka za mwisho kama watu wataitikia kwa imani.
Mwandishi
Yoeli.
Tarehe
Labda karne ya 9 K.K.
Mgawanyo
Tauni la nzige na maana yake (1:1–2:17)
Baraka za wakati huo kuahidiwa (2:18-27)
Baraka za wakati ujao kuahidiwa (2:28-32)
Hukumu ya maadui wa Israeli (3:1-21).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu