3
Yona Aenda Ninawi
1 #
Yon 1:1
Ndipo neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili: 2“Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.”
3Yona akalitii neno la Bwana naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka. 4#Yer 18:7-10#Kum 18:22Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.” 5#Mt 12:41; 11:21; Dan 9:3; Lk 11:32Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia.
6 #
Es 4:1-3; Yer 6:26; Mik 1:10; Ay 2:8-13; Eze 27:30-31; Mao 3:29 Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini. 7#2Nya 20:3; Ezr 10:6; Yoe 2:15Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote:
“Kwa amri ya mfalme na wakuu wake:
“Msiruhusu mtu yeyote au mnyama, makundi ya ng’ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu chochote, msiwaruhusu kula wala kunywa. 8#Za 130:1; Yon 1:6; Isa 1:16; Eze 33:11; Dan 4:27; Yer 25:5; 7:3; Ay 16:17Bali wanadamu na wanyama wafunikwe kwa nguo za gunia. Kila mmoja afanye hima kumwomba Mungu. Waziache njia zao mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao. 9#2Sam 12:22; Yer 18:8; Yoe 2:14; Za 85:3Ni nani ajuaye? Huenda Mungu akaghairi kwa huruma yake akaacha hasira yake kali ili tusiangamie.”
10 #
Amo 7:6; Yer 18:8; Kut 32:14 Mungu alipoona walivyofanya na jinsi walivyogeuka kutoka njia zao mbaya, akawa na huruma wala hakuleta maangamizi juu yao kama alivyokuwa ameonya.