Yona Utangulizi
NMM

Yona Utangulizi

Utangulizi
Yona alikuwa nabii aliyezaliwa Israeli (2 Wafalme 14:25), na akaitwa na Mwenyezi Mungu kuhubiri toba kule Ashuru, ufalme ambao mji mkuu ulikuwa Ninawi. Taifa hilo lilikuwa linaenda kuangamiza Israeli hivi karibuni katika 722 KK. Baada ya kupata wito, uzalendo wa Yona haungemruhusu kuwaokoa wapagani, kwa hivyo alijaribu kumkimbia Mwenyezi Mungu akitumia meli. Alitupwa baharini na akamezwa na samaki mkubwa, kisha akatupwa kwenye ufuo wa bahari na mwishowe akatii maagizo ya Mwenyezi Mungu kwa kwenda Ninawi kuhubiri. Mafanikio yake kule yalimkasirisha, lakini Mwenyezi Mungu alimfundisha somo akitumia mfano wa mmea. Kisa cha Yona ndani ya samaki kinatumika kama mfano wa mazishi ya Isa katika Injili (Mathayo 12:38-41).
Wazo Kuu
Wazo kuu katika kitabu cha Yona linapatikana katika 4:11 ambapo Mwenyezi Mungu anatangaza upendo wake kwa wanadamu wote, wawe Waisraeli au sio. Yona alishindwa kuwapenda Waashuru vizuri, lakini Mwenyezi Mungu hakutamani chochote kwao bali tu wema na wokovu wao. Hivyo alimtuma nabii kuleta toba iletayo uzima. Kitabu hiki kinaonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu na mamlaka yake juu ya nguvu za maumbile.
Mwandishi
Yona.
Tarehe
Karne ya 8 K.K.
Mgawanyo
• Yona anamkimbia Mwenyezi Mungu (1:1-17)
• Sala la Yona katika tumbo la samaki (2:1-10).
• Yona anatumwa tena, na kufanikiwa kwake (3:1-10)
• Hisia za Yona, na kujali kwa Mwenyezi Mungu (4:1-11).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu