Yoshua 12
NMM

Yoshua 12

12
Orodha Ya Wafalme Walioshindwa
1 # Za 136:21; Hes 32:19; Hes 21:13; Kum 3:8; Yos 11:2 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
2 # Yos 12:5; Hes 21:21-25; Yos 13:10; Amu 11:19; Hes 32:34; Yos 13:16; Mwa 19:38; 31:21; 32:22; Hes 32:26; Kum 2:36; 3:15; Yos 13:11, 25; 17:1; 20:8; 21:38; Amu 5:17; 7:3; 10:8 Sihoni mfalme wa Waamori,
ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 3#Yos 11:2; Mwa 14:3; Hes 33:49; Yos 13:20; Hes 21:20Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi#12:3 Yaani Bahari ya Galilaya. hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi#12:3 Yaani Bahari Mfu.), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
4 # Hes 21:21; 33; Yos 13:30; Mwa 14:5; Kum 1:4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani,
aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei. 5#Kum 3:10; Hes 32:33; Yos 17:1; 20:8; 21:27; 22:7; Yos 13:2, 13; 1Sam 27:8; Kum 3:14Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
6 # Kum 3:8; Hes 32:29-33; Yos 13:8 Musa, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Musa mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
7 # Yos 11:17 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: 8#Ezr 9:1; Kum 1:7; Yos 3:10; 11:17nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
9# Hes 33:48; Mwa 12:8; Yos 8:1; Yos 7:2; 8:9; 18:13; Amu 1:23; 4:4; 20:18; 21:2; Neh 11:31 mfalme wa Yeriko mmoja
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
10# Yos 10:1 mfalme wa Yerusalemu mmoja
mfalme wa Hebroni mmoja
11# Yos 10:3 mfalme wa Yarmuthi mmoja
mfalme wa Lakishi mmoja
12# Yos 10:3, 33 mfalme wa Egloni mmoja
mfalme wa Gezeri mmoja
13mfalme wa Debiri mmoja
mfalme wa Gederi mmoja
14# Hes 14:45; Hes 21:1 mfalme wa Horma mmoja
mfalme wa Aradi mmoja
15# Hes 33:20; Mwa 38:1; Yos 15:35; Mik 1:15 mfalme wa Libna mmoja
mfalme wa Adulamu mmoja
16# Yos 10:10; Yos 7:2 mfalme wa Makeda mmoja
mfalme wa Betheli mmoja
17# Yos 15:34; 16:8; 17:8; Yos 11:22; 1Fal 4:10 mfalme wa Tapua mmoja
mfalme wa Heferi mmoja
18# Yos 13:4; 19:30; Amu 1:31; 1Sam 4:1; 29:1 mfalme wa Afeki mmoja
mfalme wa Lasharoni mmoja
19# Yos 11:1 mfalme wa Madoni mmoja
mfalme wa Hazori mmoja
20# Yos 11:1 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja
mfalme wa Akishafu mmoja
21# Yos 17:11; 21:25; Amu 1:27; 5:19; 1Fal 4:12 mfalme wa Taanaki mmoja
mfalme wa Megido mmoja
22# Yos 15:23; 19:37; 20:7; 21:32; Amu 4:6-9; Yos 19:11; Yos 21:34; Yos 15:55; 19:26; 1Sam 15:12; 2Sam 23:35 mfalme wa Kedeshi mmoja
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
23# Yos 11:2 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori)#12:23 Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori. mmoja
mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja
24# 1Fal 14:17; 15:33; 16:8, 23; Wim 6:4; Za 135:11; 136:18 mfalme wa Tirsa mmoja
wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu