16
Mgawo Kwa Efraimu Na Manase
1 #
Yos 8:15; 12:9; 18:12 Mgawanyo wa Yusufu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli. 2#Mwa 28:19; 2Sam 15:32; Hes 32:3Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia eneo la Waariki huko Atarothi, 3#Yos 10:10; Yos 10:33; 1Fal 9:15ukateremkia kuelekea magharibi hadi eneo la Wayafleti ukienea hadi eneo la Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.
4 #
Yos 17:14; 18:5 Kwa hiyo Manase na Efraimu, wazao wa Yusufu, walipokea urithi wao.
5 #
Yos 18:13; 10:10 Hili ndiyo lilikuwa eneo la Efraimu, ukoo kwa ukoo:
Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu, 6#Yos 17:7; 2Fal 15:29na kuendelea mpaka baharini. Kutoka Mikmeta upande wa kaskazini ulipinda kuelekea mashariki hadi Taanath-Shilo, ukiupita hadi Yanoa upande wa mashariki. 7#Hes 32:3Kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara, ukagusa Yeriko na kutokea katika Mto Yordani. 8#Yos 12:17; 17:9; 19:28Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo. 9#Eze 48:5Pia ulijumuisha miji yote na vijiji vyake ambavyo vilitengwa kwa ajili ya Waefraimu ndani ya urithi wa kabila la Manase.
10 #
Yos 15:63; 17:12-13; Amu 1:28-29; 1Fal 9:16 Hawakuwatoa Wakanaani waishio Gezeri; mpaka leo Wakanaani wanaishi miongoni mwa watu wa Efraimu lakini wanatakiwa kufanya za kulazimishwa.