Yoshua 24
NMM

Yoshua 24

24
Agano Lafanywa Upya Huko Shekemu
1 # Mwa 49:2; Mwa 12:6; 1Sam 12:7; 1Fal 8:14; Yos 7:6; 23:2; Amu 9:1-3; Kut 18:25; 1Sam 10:10; Mdo 10:33 Ndipo Yoshua akaita pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu. Akawaita wazee, viongozi, waamuzi na maafisa wa Israeli, nao wakaja mbele za Mungu.
2 # Mwa 23:2; Mwa 11:32; Kum 26:5; Isa 51:2 Yoshua akawaambia watu wote, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Hapo zamani baba zenu, pamoja na Tera baba yake Ibrahimu na Nahori, waliishi ng’ambo ya Mto nao waliiabudu miungu mingine. 3#Mwa 12:1; Mwa 1:28; 12:2; 21:3; Mdo 7:2; Za 127:3Lakini nilimwondoa baba yenu Ibrahimu kutoka nchi hiyo ng’ambo ya Mto, nami nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani, nikampa wazao wengi. Nikampa Isaka, 4#Mwa 25:26; Mwa 14:6; Hes 24:18; Mwa 46:5-6; Kum 2:5; Mdo 17:26naye Isaka nikampa Yakobo na Esau. Esau nikampa nchi ya vilima ya Seiri, lakini Yakobo pamoja na wanawe wakashuka Misri.
5 # Kut 3:10; Kut 12:51 “ ‘Kisha nikawatuma Musa na Haruni, nami nikawapiga Wamisri kwa kile nilichokitenda huko, tena nikawatoa ninyi huko. 6#Kut 14:22; Kut 14:9; Kut 4:23; Mik 6:4; Neh 9:11; Za 78:13; Isa 63:12, 13Nilipowatoa baba zenu Misri, mlifika kwenye bahari, nao Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka kwenye Bahari ya Shamu. 7#Kut 14:10, 20, 28; Kut 19:4; Kum 1:46Lakini wakamlilia Bwana wakitaka msaada, naye akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao ikawafunika. Ninyi mliona kwa macho yenu wenyewe kile nilichowatendea Wamisri. Kisha mliishi jangwani kwa muda mrefu.
8 # Kut 23:23; Hes 21:31 “ ‘Nikawaleta katika nchi ya Waamori ambao waliishi mashariki mwa Yordani. Wakapigana nanyi, lakini nikawatia mikononi mwenu. Nikawaangamiza mbele yenu nanyi mkaimiliki nchi yao. 9#Hes 22:2, 6; Hes 23:7Wakati Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, alipojiandaa kupigana dhidi ya Israeli, alimwita Balaamu mwana wa Beori apate kuwalaani. 10#Hes 23:10; Kum 23:5Lakini sikumkubali Balaamu, kwa hiyo aliwabariki tena na tena, nami niliwaokoa toka mkononi mwake.
11 # Kut 14:29; Yos 6:1; 3:10; Mwa 15:18-21; Kut 23:23; Kum 7:1 “ ‘Ndipo mlipovuka Yordani mkafika Yeriko. Raiya wa Yeriko wakapigana nanyi, kama walivyofanya Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi, lakini niliwatia mikononi mwenu. 12#Kut 23:28; Za 44:3-7; Kut 23:31; Za 135:11; Kum 7:20Nikatuma manyigu mbele yenu, ambao pia waliwafukuza mbele yenu, hao wafalme wawili wa Waamori. Siyo upanga au upinde wenu wenyewe vilivyowapatia ushindi. 13#Kut 6:8; Kum 6:10-11; Yos 11:13; Mit 13:22Hivyo nikawapa ninyi nchi ambayo hamkuitaabikia na miji ambayo hamkuijenga na mnaishi ndani yake na kula toka kwa mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.’
14 # 1Sam 12:14; Ay 23:15; Za 19:9; 119:120; Kum 10:12; 18:13; 1Sam 12:24; 2Kor 1:20; Mwa 31:19; Kut 12:12; 18:11; 20:3; Hes 25:2; Kum 11:28; Amu 10:16; Amu 10:16; Rut 1:15; Isa 55; 7; Eze 23; 3 “Sasa basi mcheni Bwana na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ng’ambo ya Mto Frati na huko Misri, nanyi mtumikieni Bwana. 15#Amu 6:10; Rut 1:15-16; Rut 2:12; Mwa 35:2; 1Fal 18:21; Dan 3:18Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana.”
16 # Yos 22:29 Ndipo hao watu wakajibu, “Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Bwana na kuitumikia miungu mingine! 17#Amu 6:8; Kut 10:1Bwana Mwenyezi Mungu wetu mwenyewe ndiye alitutoa sisi na baba zetu akatupandisha kutoka Misri, kutoka nchi ile ya utumwa, na kutenda zile ishara kubwa mbele ya macho yetu. Ndiye aliyetulinda katika safari yetu yote na kutokana na mataifa yote ambayo tulipita katikati yao. 18#Kut 23:31; Kum 33:27; Mdo 7:45; Mwa 28:21Bwana akayafukuza mbele yetu mataifa yote pamoja na Waamori, walioishi katika nchi hii. Hivyo sisi nasi tutamtumikia Bwana kwa kuwa yeye ndiye Mungu wetu.”
19 # Law 11:44; 20:26; Kut 20:5; 34:7; Kut 23:21; Rut 1:15; Mt 6:24; Lk 14:25-33; Law 19:2; 1Sam 6:20; Za 99:5, 9; Isa 5:16; Kut 23:21 Yoshua akawaambia watu, “Hamwezi kumtumikia Bwana. Yeye ni Mungu Mtakatifu, ni Mungu mwenye wivu. Hatasamehe uasi wenu na dhambi zenu. 20#1Nya 28:9, 20; 2Nya 24:18; Mdo 7:42; 1Sam 12:25; Hos 13:11; Yos 23:15; Ezr 8:22; Isa 1:28; 63:10; Yer 17:13; Ebr 10:26-28Ikiwa mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, atageuka na kuwaleteeni maafa na kuwaangamiza, baada ya kuwa mwema kwenu.”
21Lakini watu wakamwambia Yoshua, “Sivyo! Sisi tutamtumikia Bwana.”
22 # Rut 2:10; Isa 8; 2; 43:10; 44:8; Yer 42:5; Mal 2:14; Za 119:30, 173; Kum 25:9 Ndipo Yoshua akawaambia, “Ninyi mmekuwa mashahidi juu yenu wenyewe kuwa mmechagua kumtumikia Bwana.”
Nao wakajibu, “Ndiyo, tu mashahidi.”
23 # 1Fal 8:58; Za 119:36; 141:4; Yer 31:33 Yoshua akawaambia, “Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni iliyo katikati yenu, nanyi mtoleeni Bwana, Mungu wa Israeli, mioyo yenu.”
24 # Kut 19:8; Yer 42:6 Nao watu wakamwambia Yoshua, “Tutamtumikia Bwana Mwenyezi Mungu wetu na kumtii yeye.”
25 # Kut 24:8; Yos 17:7; Kut 15:25 Siku ile Yoshua akafanya agano kwa ajili ya watu na hapo Shekemu ndipo alipowaandikia amri na sheria. 26#Kum 17:18; 28:61; 31:24; Mwa 28:18; Kum 27:2; Mwa 12:6; Amu 4:11Naye Yoshua akayaandika mambo haya katika Kitabu cha Sheria ya Mungu. Ndipo akalitwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko chini ya mwaloni, karibu na mahali patakatifu pa Bwana.
27 # Mwa 28:18; Mwa 21:30; Yos 22:27; Yos 7:11; Hes 11:20; Mit 30:9 Yoshua akawaambia watu wote, “Angalieni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yote Bwana aliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.”
Kuzikwa Katika Nchi Ya Ahadi
28 # Amu 21:23-24 Basi Yoshua akawatuma watu kila mmoja aende katika urithi wake mwenyewe.
29 # Amu 1:1; Mwa 50:22 Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. 30#Yos 19:50; 2Sam 23:30; Amu 2:7Nao wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Sera#24:30 Unajulikana pia kama Timnath-Heresi, ona Yos 19:50; Amu 2:9. katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima wa Gaashi.
31 # Yos 7:6 Israeli wakamtumikia Bwana siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, ambao waliona kila kitu Bwana alichowatendea Israeli.
32 # Ebr 11:22; Mwa 47:29-30; Mwa 33:19; Yn 4:6; Mdo 7:16; Mwa 50:25; Kut 13:19 Nayo ile mifupa ya Yusufu, ambayo Waisraeli waliipandisha kutoka huko Misri, wakaizika huko Shekemu kwenye eneo, ambalo Yakobo alilinunua kwa wana wa Hamori baba yake Shekemu, kwa vipande mia vya fedha. Eneo hili likawa ni urithi wa uzao wa Yusufu.
33 # Yos 22:13; 15:57; Kut 6:25; 1Sam 9:4; 1Fal 8:4; Kut 6:25; Amu 20:28 Naye Eleazari mwana wa Haruni akafariki akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu