Utangulizi
Baada ya kifo cha Musa, uongozi wa taifa ulichukuliwa na Yoshua, naye akawa amri jeshi wao wakati wote wa vita Israeli ilipokuwa inanyakua nchi. Yoshua alihamasisha majeshi yake wakiwa bado katika nchi tambarare ya Moabu na kuwaandaa kwa vita. Baada ya hapo walivuka Mto Yordani na vita vikaanza. Kulikuwa na harakati tatu za mapigano, moja sehemu ya kaskazini, moja eneo la kati, na nyingine eneo la kusini. Zote zimeelezewa, lakini kwa kiasi tu. Baada ya ushindi wa mwanzo, nchi iligawanywa kwa makabila ya Israeli. Kisha Yoshua akawahimiza watu na kufariki kwa amani.
Wazo Kuu
Kitabu cha Yoshua kinaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu hutimiza ahadi zake. Aliwaahidi watu wake nchi, na sasa walikuwa wanaingia kuimiliki. Lakini sio bila jitihada zozote: Mwenyezi Mungu aliwataka kujihusisha na vita ili wapate kile alichokuwa amewapa. Hukumu ya Mwenyezi Mungu juu ya dhambi za Wakanaani kwa njia ya majeshi ya Israeli pia ni jambo muhimu.
Mwandishi
Labda Yoshua.
Tarehe
Karne ya 14 au ya 12 KK.
Mgawanyo
• Kuhamasishana kuvuka nchi ya Kanaani (1:1–5:15)
• Harakati za kati (6:1–8:35)
• Harakati za kusini (9:1–10:43)
• Harakati za kaskazini (11:1-15)
• Muhtasari na mgawanyo wa nchi kwa makabila (11:16–22:34)
• Maneno ya mwisho ya Yoshua, na kifo chake (23:1–24:33).