Maombolezo 5
NMM

Maombolezo 5

5
1 # Za 44:13-16; Za 89:50 Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata,
tazama, nawe uione aibu yetu.
2 # Za 79:1; Sef 1:13; Yer 17:4 Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni,
na nyumba zetu kwa wageni.
3 # Kut 22:24; Yer 15:8; Yer 18:21 Tumekuwa yatima wasio na baba,
mama zetu wamekuwa kama wajane.
4 # Isa 55:1; Eze 4:16-17; Isa 3:1 Ni lazima tununue maji tunayokunywa,
kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.
5 # Isa 47:6; Neh 9:37; Yos 1:13 Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu,
tumechoka na hakuna pumziko.
6 # Yer 2:36; Mwa 24:2; Hos 5:13; 7:11; Yer 50:15; Hos 12:1 Tumejitolea kwa Misri na Ashuru
tupate chakula cha kutosha.
7 # Yer 14:20; 16:12; Eze 8:2; Yer 31:29; Eze 18:2; Mt 23:32 Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena,
na sisi tunachukua adhabu yao.
8 # Neh 5:15; Zek 11:6 Watumwa wanatutawala
na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
9Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu
kwa sababu ya upanga jangwani.
10 # Ay 30:30; Mao 4:8-9 Ngozi yetu ina joto kama tanuru,
kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
11 # Mwa 34:29; Zek 14:2; Isa 13:16 Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni,
na mabikira katika miji ya Yuda.
12Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao,
wazee hawapewi heshima.
13 # Amu 13:16; Amu 16:21 Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia,
wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.
14 # Isa 24:8; Yer 7:34; 2Fal 25:18 Wazee wameondoka langoni la mji,
vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
15 # Amu 8:10; Yer 25:10 Furaha imeondoka mioyoni mwetu,
kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
16 # Yer 13:18; Yer 14:20; Za 89:39; Ay 19:9; Isa 3:11 Taji imeanguka kutoka kichwani petu.
Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!
17 # Ay 17:7; Za 6:7; 16:8; Yer 8:18 Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia,
kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,
18 # Isa 27:10; Mik 3:12; Za 74:2-4 kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa,
nao mbweha wanatembea juu yake.
19 # 1Nya 16:31; Za 45:6; Za 102:22-27 Wewe, Ee Bwana unatawala milele,
kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.
20 # Za 13:1; 44:24; 71:11 Kwa nini watusahau siku zote?
Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu?
21 # Isa 60:20-22; Za 80:3 Turudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana,
ili tupate kurudi.
Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale,
22 # Isa 64:9; Yer 6:30; Za 53:5; 60:12 isipokuwa uwe umetukataa kabisa
na umetukasirikia pasipo kipimo.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu