Utangulizi
Kitabu cha Mambo ya Walawi kiliandikwa kiwe kitabu cha maelekezo kwa makuhani au Walawi, hivyo kinaitwa Mambo ya Walawi. Kitabu hiki kinatoa maagizo na sheria ambazo zingeongoza Israeli kwa ujumla, na hasa kuwapa sheria kuhusu dhabihu na ibada. Dhabihu nyingine muhimu zimeelezewa, na pia jinsi zingetolewa. Sherehe zote muhimu zimeelezewa. Pia kuna sehemu maalumu zilizoeleza kuhusu ukuhani, na sheria kuhusu mambo ya sherehe.
Wazo Kuu
Wazo kuu katika kitabu hiki ni kwamba Mwenyezi Mungu ametoa njia ya upatanisho kufanyika kwa kutoa dhabihu ya damu. Mfumo huu ulipata utimilifu katika umwagaji wa damu ya Al-Masihi kama sadaka moja kuu kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Kitabu cha Mambo ya Walawi pia kinaonyesha kuwa lazima ibada iwe na utaratibu na ifuate ratiba.
Mwandishi
Musa.
Tarehe
Kama 1420 au 1220 K.K.
Mgawanyo
• Mfumo wa dhabihu (1:1–15:33)
• Siku kuu ya Upatanisho (16:1-34)
• Sheria tofauti (17:1–20:27)
• Sheria kwa makuhani (21:1–22:33)
• Sheria kuhusu sherehe mbalimbali (23:1–25:55)
• Utiifu, viapo, na zaka (26:1–27:34).