Luka 17
NMM

Luka 17

17
Isa Afundisha Kuhusu Majaribu, Dhambi Na Imani
(Mathayo 18:6-7, 21-22; Marko 9:42)
1 # Mt 5:29; 18:7 Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. 2#Mk 10:24; Lk 10:21; Mt 5:29Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, kuliko kumsababisha mmojawapo wa hawa wadogo kutenda dhambi. 3#Mt 18:15; Efe 4:32; Kol 3:13Kwa hiyo, jilindeni.
“Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu, msamehe. 4#Mt 18:21-22Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe.”
Imani
5 # Mk 6:30; Lk 7:13 Mitume wake wakamwambia Bwana, “Tuongezee imani.”
6 # Mt 13:31; Mt 17:20; 21:21; Mk 9:23 Bwana akawajibu, “Kama mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.
Wajibu Wa Mtumishi
7“Ikiwa mmoja wenu ana mtumishi anayelima shambani au anayechunga kondoo, je, mtumishi huyo arudipo atamwambia, ‘Karibu hapa keti ule chakula?’ 8#Lk 12:37Je, badala yake, hatamwambia, ‘Niandalie chakula, nile, jifunge unitumikie ninapokula na kunywa; baadaye waweza kula na kunywa?’ 9Je, huyo mtu atamshukuru mtumishi huyo kwa kutimiza yale aliyoamriwa? 10#1Kor 9:16Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’ ”
Isa Atakasa Wakoma Kumi
11 # Lk 9:51-52; Yn 4:3-4 Isa alipokuwa njiani akienda Yerusalemu, alipitia mpakani mwa Samaria na Galilaya. 12#Mt 8:2; Law 13:45-46Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, 13#Lk 5:5wakapaza sauti, wakasema, “Isa, Bwana, tuhurumie!”
14 # Law 14:2; Mt 8:4 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.
15 # Mt 9:8 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Isa, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 16#Mt 10:5Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.
17Isa akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?” 19#Mt 9:22Isa akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.”
Kuja Kwa Ufalme Wa Mungu
(Mathayo 24:23-28, 37-41)
20 # Yn 18:36; 3:3 Isa alipoulizwa na Mafarisayo Ufalme wa Mungu utakuja lini, yeye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuchunguza kwa bidii, 21#Mt 24:23; Yn 1:26; 12:35wala watu hawatasema, ‘Huu hapa,’ au ‘Ule kule,’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
22 # Mt 8:20; Mt 9:15; Lk 5:35 Kisha Isa akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. 23#Mt 24:23; Mk 13:21Watu watawaambia, ‘Yule kule!’ Au, ‘Huyu hapa!’ Msiwakimbilie. 24#Mt 24:27Kwa maana kama vile umeme wa radi umulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. 25#Mt 16:21; Lk 9:22; Mk 13:30; Lk 18:32Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.
26 # Mwa 6:5-8; Mwa 7:6-24 “Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. 27#Mwa 7:7-23Watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo gharika ikaja na kuwaangamiza wote.
28 # Mwa 19:1-28 “Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Lutu: Watu walikuwa wakila na kunywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga. 29#Mwa 19:1-28Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza wote.
30 # 2Pet 3:4; Ufu 1:7 “Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. 31#Mt 24:17-18; Mk 13:15-16Siku hiyo, mtu yeyote aliye juu ya dari ya nyumba yake, hata vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba, asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua chochote. 32#Mwa 19:26Mkumbukeni mke wa Lutu! 33#Yn 12:25Mtu yeyote anayejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa. 34#Mt 24:40, 41; 1The 4:17Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. 35#Mt 24:41Wanawake wawili watakuwa wanasaga nafaka pamoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. [36Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.]”
37 # Mt 24:28 Kisha wakamuuliza, “Haya yatatukia wapi Bwana?”
Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, huko ndiko tai watakapokusanyika.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu