Mathayo 11
NMM

Mathayo 11

11
Isa Na Yahya Mbatizaji
(Luka 7:18-35)
1 # Mt 7:28; 26:1 Baada ya Isa kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.
2 # Mt 14:3 Yahya aliposikia akiwa gerezani mambo ambayo Al-Masihi#11:2 Al-Masihi maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. alikuwa akiyafanya, aliwatuma wanafunzi wake 3#Za 118:26; Ebr 10:37ili wakamuulize, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”
4Isa akajibu, “Rudini mkamwambie Yahya yale mnayosikia na kuyaona: 5#Lk 4:18-19; Isa 61:1-2Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. 6#Mt 13:21; 26:31Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”
7 # Mt 3:1-5 Wale wanafunzi wa Yahya walipokuwa wanaondoka, Isa akaanza kusema na makutano kuhusu Yahya Mbatizaji. Akawauliza, “Mlipokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? 8Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya kifahari wako katika majumba ya wafalme. 9#Lk 1:76; 7:26Basi mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. 10#Mal 3:1; Lk 7:27Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:
“ ‘Tazama nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako.’
11 # Mt 13:17 Amin, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu kuliko Yahya Mbatizaji. Lakini aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni ni mkuu kuliko Yahya. 12#Lk 16:16; 13:24Tangu siku za Yahya Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka. 13#Lk 16:16Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yahya. 14#Mal 4:5; Yn 1:21Ikiwa mko tayari kukubali hilo, yeye (Yahya) ndiye yule Ilya ambaye manabii walikuwa wamesema angekuja. 15#Lk 14:35; Ufu 2:7Yeye aliye na masikio, na asikie.
16 # Lk 7:31 “Lakini kizazi hiki nikifananishe na nini? Kinafanana na watoto waliokaa sokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia,
17 # Mit 29:9 “ ‘Tuliwapigia filimbi,
lakini hamkucheza;
tuliwaimbia nyimbo za maombolezo,
lakini hamkuomboleza.’
18 # Mt 3:4; Lk 1:15 Kwa maana Yahya Mbatizaji alikuja, alikuwa hali wala hanywi, nao wanasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’ 19#Mt 9:11Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.”
Onyo Kwa Miji Isiyotubu
(Luka 10:13-15)
20 # Lk 10:11 Ndipo Isa akaanza kushutumu miji ambamo alifanya miujiza yake mingi kuliko kwingine, kwa maana watu wake hawakutubu. 21#Mk 8:22; Yn 1:44; Yoe 3:4; Mk 3:8; Yn 3:5-9“Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. 22#Mt 11:24; 10:15Lakini nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili katika siku ya hukumu, kuliko ninyi. 23#Mt 4:13; Isa 14:13-15Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu.#11:23 Kuzimu ni Mahali pa wafu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwepo hadi leo. 24#Mt 10:15Lakini nakuambia kwamba, itakuwa rahisi zaidi kwa Sodoma kustahimili katika siku ya hukumu kuliko wewe.”
Hakuna Amjuaye Baba Ila Mwana
(Luka 10:21-22)
25 # Lk 23:34; Yn 12:27-28; Mt 13:11; 1Kor 1:26-29 Wakati huo Isa alisema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. 26Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.
27 # Mt 28:18; Yn 3:35; 10:15; 17:25-26 “Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.
Isa Awaita Waliolemewa Na Mizigo
28 # Yn 7:37 “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29#Flp 2:5; 1Yn 2:6; Za 116:7; Yer 6:16Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30#1Yn 5:3Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu