14
Yahya Mbatizaji Akatwa Kichwa
(Marko 6:14-29; Luka 9:7-9)
1 #
Lk 13:31; 9:7-9; Mdo 12:1 Wakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Isa, 2#Mt 3:1akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yahya Mbatizaji; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”
3 #
Mt 4:12; 11:2; Lk 3:19-20 Herode alikuwa amemkamata Yahya, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, 4#Law 18:16; 20:21kwa kuwa Yahya alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” 5#Mt 11:19; Mt 21:26; Lk 20:26Herode alitaka sana kumuua Yahya, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.
6Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode, 7kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba. 8Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yahya Mbatizaji kwenye sinia.” 9Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. 10#Mt 17:12Hivyo akaagiza Yahya Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani. 11Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake. 12#Mt 8:2Wanafunzi wa Yahya wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Isa.
Isa Alisha Wanaume 5,000
(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14)
13 #
Mk 6:31-44; Mt 10:23; Mk 6:32; Lk 9:19; Yn 6:13 Isa aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. 14#Mt 9:36; 4:23Isa alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.
15 #
Mk 6:35; Lk 9:12; Yn 6:5 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”
16Isa akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.”
17 #
Mt 16:9; 1Sam 9:13; 1Kor 10:16 Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”
18Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” 19#Mt 15:36; 1Sam 9:13; Mt 26:26; Mk 8:6; Lk 9:16; 24:30; Mdo 2:42; 20:7Isa akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano. 20#2Fal 4:44Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Isa Atembea Juu Ya Maji
(Marko 6:45-52; Yohana 6:15-21)
22 #
Mk 6:45-46
Mara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda ng’ambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 23#Lk 3:21; Lk 6:12; 9:18Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Isa alikuwa huko peke yake. 24Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
25Wakati wa zamu ya nne ya usiku,#14:25 Zamu ya nne ya usiku ni kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi. Isa akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26#Lk 24:37; Ay 9:8Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.
27 #
Mt 9:2; Mdo 23:11; Dan 10:12; Mdo 18:9 Lakini mara Isa akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”
28Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.”
29Isa akamwambia, “Njoo.”
Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Isa. 30Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”
31 #
Mt 6:30
Mara Isa akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?”
32Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma. 33#Za 2:7; Mt 4:3Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Isa, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
Isa Awaponya Wagonjwa Genesareti
(Marko 6:53-56)
34Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti. 35Watu wa eneo lile walipomtambua Isa, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote, 36#Mt 9:20-21wakamsihi awaruhusu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake, nao wote waliomgusa, wakaponywa.