Mathayo 26
NMM

Mathayo 26

26
Shauri Baya La Kumuua Isa
(Marko 14:1-2; Luka 22:1-2; Yohana 11:45-53)
1 # Mt 7:28 Isa alipomaliza kusema hayo yote, akawaambia wanafunzi wake, 2#Yn 11:55; 13:1“Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.”
3 # Za 2:2; Lk 3:2; Mdo 4:6 Basi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa. 4#Mt 12:14Wakafanya shauri ili kumkamata Isa kwa siri na kumuua. 5#Mt 27:24Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”
Isa Anapakwa Mafuta Huko Bethania
(Marko 14:3-9; Yohana 12:1-8)
6 # Mt 21:17 Isa alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma, 7naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Isa alipokuwa ameketi mezani kula chakula.
8 # Yn 12:4 Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini? 9Manukato haya yangeuzwa kwa bei kubwa, na fedha hizo wakapewa maskini.”
10 # Lk 11:7 Isa, akijua jambo hili, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Yeye amenitendea jambo zuri sana. 11#Kum 15:11Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. 12#Yn 19:40Alipomiminia haya manukato kwenye mwili wangu, amefanya hivyo ili kuniandaa kwa ajili ya maziko yangu. 13Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
Yuda Akubali Kumsaliti Isa
(Marko 14:10-11; Luka 22:3-6)
14 # Mt 26:25, 47; 10:4 Kisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani 15#Kut 21:32; Zek 11:12na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Isa mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 16#1Tim 6:9, 10Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Isa.
Isa Ala Pasaka Pamoja Na Wanafunzi
(Marko 14:12-21; Luka 22:7-23; Yohana 13:21-30)
17 # Kut 12:18-20 Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimjia Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
18 # Mk 14:35, 41; Yn 17:1 Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini, mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ” 19Hivyo wanafunzi wakafanya kama vile Isa alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka.
20 # Mk 14:17-21; Lk 22:14 Ilipofika jioni, Isa alikuwa ameketi mezani pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. 21#Lk 22:21-23; Yn 13:21Nao walipokuwa wakila, Isa akasema, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”
22Wakahuzunika sana, wakaanza kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”
23 # Za 41:9; Yn 13:18 Isa akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami ndiye atakayenisaliti. 24#Dan 9:24; 1Pet 1:10-11Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!”
25 # Mt 23:7 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, akasema, “Je, ni mimi Rabi?”
Isa akajibu, “Naam, wewe mwenyewe umesema.”
Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana
(Marko 14:22-26; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)
26 # Mt 14:9; 1Kor 10:16 Walipokuwa wanakula, Isa akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu.”
27 # Mk 14:23 Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, “Nyweni nyote katika kikombe hiki. 28#Mal 2:5; Ebr 10:29; Mt 20:28; Mk 1:4Hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 29#Mdo 10:41Lakini ninawaambia, tangu sasa sitakunywa tena katika uzao huu wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”
30 # Mt 21:1; Mk 14:26 Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.
Isa Atabiri Petro Kumkana
(Marko 14:27-31; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)
31 # Mt 11:6; 13:21; Zek 13:7; Yn 16:32 Kisha Isa akawaambia, “Usiku huu, ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa:
“ ‘Nitampiga mchungaji,
nao kondoo wa hilo kundi watatawanyika.’
32 # Mt 28:7, 10, 16 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
33Petro akajibu, “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.”
34 # Yn 13:38 Isa akamjibu, “Amin, nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
35 # Yn 13:37 Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wanafunzi wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.
Isa Anaomba Gethsemane
(Marko 14:32-42; Luka 22:39-46)
36 # Mk 14:32, 35; Lk 22:39; Yn 18:1 Kisha Isa akaenda pamoja na wanafunzi wake mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia, “Kaeni hapa, nami niende kule nikaombe.” 37#Mt 4:21Akamchukua Petro pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kufadhaika. 38#Yn 12:27Kisha Isa akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe pamoja nami.”
39 # Mt 20:22; Za 40:6-8; Yn 4:34 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniondokee. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali kama upendavyo wewe.”
40 # Mt 26:38 Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamuuliza Petro, “Je, ninyi hamkuweza kukesha pamoja nami hata kwa saa moja? 41#Mt 6:13Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”
42 # Mt 26:39 Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.”
43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44#2Kor 12:8Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale.
45 # Mt 26:18 Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Tazameni, saa imefika ambapo Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. 46#Yn 14:31Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”
Isa Akamatwa
(Marko 14:43-50; Luka 22:47-53; Yohana 18:3-12)
47 # Mt 10:4 Alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale Kumi na Wawili, akafika. Alikuwa amefuatana na umati mkubwa wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 48Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni.” 49#Mt 23:7Mara Yuda akamjia Isa na kumsalimu, “Salamu, Rabi!” Akambusu.
50 # Mt 20:13; 22:12 Isa akamwambia, “Rafiki, fanya kile ulichokuja kufanya hapa.”
Kisha wale watu wakasogea mbele, wakamkamata Isa. 51#Lk 22:36-38; Yn 18:10Ghafula mmoja wa wale waliokuwa na Isa alipoona hivyo, akaushika upanga wake, akauchomoa na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
52 # Kut 21:12; Ufu 13:10 Ndipo Isa akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. 53#2Fal 6:17; Mt 4:11Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? 54#Mt 1:22; 26:24Lakini je, yale Maandiko yanayotabiri kwamba ni lazima itendeke hivi yatatimiaje?”
55 # Lk 21:27; Yn 18:20 Wakati huo, Isa akawaambia ule umati wa watu, “Je, mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi? Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata? 56#Mt 26:31Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia.
Isa Mbele Ya Kuhani Mkuu
(Marko 14:53-65; Luka 22:54-71; Yohana 18:13-24)
57 # Mk 14:53; Lk 22:54; Yn 18:12; 13:14 Wale waliokuwa wamemkamata Isa wakampeleka kwa Kayafa, kuhani mkuu, mahali ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika. 58#Mk 14:66; 15:16; Lk 22:55; 11:21Lakini Petro akamfuata kwa mbali hadi uani kwa kuhani mkuu. Akaingia ndani, akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.
59 # Mt 5:22 Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Isa ili wapate kumuua. 60#Za 27:12; Mdo 6:13; Kum 19:15Lakini hawakupata jambo lolote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza.
Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo 61#Yn 2:19na kusema, “Huyu mtu alisema, ‘Ninaweza kulivunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’ ”
62 # Mk 14:60 Kisha kuhani mkuu akasimama na kumwambia Isa, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” 63#Mt 27:12-14; Mk 14:61; Dan 7:13Lakini Isa akakaa kimya.
Ndipo kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai. Tuambie kama wewe ndiwe Al-Masihi,#26:63 Al-Masihi maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu.”
64 # Dan 7:13; Mt 16:27; 24:30; Lk 21:27 Isa akajibu, “Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote: Siku za baadaye, mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
65 # Mk 14:63 Ndipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru. 66#Law 24:16; Yn 19:7Uamuzi wenu ni gani?”
Wakajibu, “Anastahili kufa.”
67 # Mt 16:21; Mt 27:30 Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi 68#Lk 22:63-65na kusema, “Tutabirie, wewe Al-Masihi! Ni nani aliyekupiga?”
Petro Amkana Bwana Isa
(Marko 14:66-72; Luka 22:56-62; Yohana 18:15-18, 25-27)
69 # Mk 14:66; Lk 22:55; Yn 18:16, 17, 25 Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Isa wa Galilaya.”
70Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.”
71Alipotoka nje kufika kwenye lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwepo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Isa, Mnasiri.”
72Akakana tena kwa kiapo akisema, “Mimi simjui huyo!”
73 # Lk 22:59 Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.”
74 # Mk 14:71 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui mtu huyo!”
Papo hapo jogoo akawika. 75#Mt 26:24; Yn 13:38Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alilokuwa amesema: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu