Mathayo 3
NMM

Mathayo 3

3
Yahya Mbatizaji Atayarisha Njia
(Marko 1:1-8; Luka 3:1-18; Yohana 1:19-28)
1 # Lk 3:2-19 Siku hizo Yahya Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Uyahudi, akisema, 2#Dan 7:14; Lk 17:20“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.” 3#Mal 3:1; Yn 1:23Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema:
“Sauti ya mtu aliaye huko nyikani,
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.’ ”
4 # 1Fal 1:8 Basi Yahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5#Mk 1:5; Lk 3:7Watu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani. 6#Mdo 19:4, 18; Mk 1:4Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani.
7 # Mt 12:34; 23:33; Rum 1:18; 1The 1:10 Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8#Mdo 26:20Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. 9#Rum 2:28-29Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwa mawe haya. 10#Lk 3:9; Yn 15:2-6Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni.
11 # Mk 1:18; Isa 4:4; Mdo 2:3-4 “Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu#3:11 …kwa Roho Mtakatifu hapa ina maana ya katika Roho Mtakatifu. na kwa moto. 12#Mt 13:30; 25:41Pepeto lake liko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, na kuikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.”
Isa Abatizwa
(Marko 1:9-11; Luka 3:21-22)
13 # Mt 3:1; Mk 1:4; Yn 1:31-34 Kisha Isa akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yahya ambatize. 14Lakini Yahya akajitahidi kumzuia, akimwambia, “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?”
15Lakini Isa akamjibu, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote.” Hivyo Yahya akakubali.
16 # Isa 11:2; 42:1; Mk 1:10; Lk 3:22; Yn 1:32-33 Naye Isa alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. 17#Kum 4:12; Yn 12:28; Za 2:7; 2:7; Mdo 13:33; Isa 42:1; 2Pet 1:17Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu