Mathayo 9
NMM

Mathayo 9

9
Isa Amponya Mtu Aliyepooza
(Marko 2:1-12; Luka 5:17-26)
1 # Mt 4:13 Isa akaingia kwenye chombo, akavuka na kufika katika mji wa kwao. 2#Mt 4:24; Mt 9:22; Yn 16:33; Lk 7:48Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa.”
3 # Mt 26:65; Yn 10:33; Mk 2:7 Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa sheria wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!”
4 # Za 94:11; Yn 2:22 Lakini Isa akiyafahamu mawazo yao, akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’? 6#Mt 9:22Lakini, ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Ndipo akamwambia yule aliyepooza, “Inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.” 7Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani kwake. 8#Yn 15:8; Mdo 4:21Makutano walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu ambaye alikuwa ametoa mamlaka kama haya kwa wanadamu.
Kuitwa Kwa Mathayo
(Marko 2:13-17; Luka 5:27-32)
9 # Mt 4:19 Isa alipokuwa akienda kutoka huko, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Isa akamwambia, “Nifuate.” Mathayo akaondoka, akamfuata.
10Isa alipokuwa akila chakula ndani ya nyumba ya Mathayo, watoza ushuru wengi na “wenye dhambi” wakaja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11#Lk 19:7; Gal 2:15Mafarisayo walipoona mambo haya, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini Mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”
12Lakini Isa aliposikia hayo, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, lakini wale walio wagonjwa ndio wanaohitaji tabibu. 13#Mik 6:6-8; Mt 12:7; Lk 19:10; 1Tim 1:15Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya: ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”
Isa Aulizwa Kuhusu Kufunga
(Marko 2:18-22; Luka 5:33-39)
14 # Mt 11:18-19; Lk 18:12 Wanafunzi wa Yahya Mbatizaji wakaja na kumuuliza Isa, “Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
15 # Yn 3:29; Mdo 13:2-3; 14:23 Isa akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.
16 # Yn 1:17 “Hakuna mtu anayeshonea kiraka kipya kwenye nguo iliyochakaa, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye hiyo nguo, nayo hiyo nguo itachanika zaidi. 17Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama wakifanya hivyo, viriba vitapasuka nayo divai itamwagika, navyo viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya, na hivyo divai na viriba huwa salama.”
Mwanamke Aponywa
(Marko 5:21-43; Luka 8:40-56)
18 # Mt 8:2; Mk 5:23 Isa alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai.” 19Isa akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye.
20 # Mk 6:56; Lk 6:19 Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Isa, akagusa upindo wa vazi lake, 21#Mt 14:36kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.”
22 # Lk 17:19; 18:42; Mt 15:28 Isa akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile.
Isa Amfufua Binti Wa Kiongozi Wa Sinagogi
23 # 2Nya 35:25; Yer 9:17-18 Isa alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele, 24#Mdo 20:10; Dan 12:2; 1The 4:13-16; Yn 11:11akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. 25#Lk 7:14Lakini watu walipokwisha kutolewa nje, akaingia mle ndani na kumshika yule binti mkono, naye akaamka. 26#Mk 1:28, 45; Lk 5:15Habari hizi zikaenea katika maeneo yale yote.
Isa Awaponya Vipofu
27 # Mk 10:47; Lk 18:38-39 Isa alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipiga kelele kwa nguvu na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!”
28 # Mdo 14:19 Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Isa akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?”
Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.”
29 # Mt 8:11; 9:22 Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.” 30#Mt 8:4Macho yao yakafunguka. Isa akawaonya vikali, akisema, “Angalieni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.” 31#Mt 9:26; Mk 7:36Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.
Isa Amponya Mtu Bubu
32 # Mt 4:24; 12:22-24 Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa. 33#Mk 2:12Yule pepo mchafu alipotolewa, yule mtu aliyekuwa bubu akaongea. Ule umati wa watu ukastaajabu na kusema, “Jambo kama hili kamwe halijapata kuonekana katika Israeli.”
34 # Mt 12:24 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa mkuu wa pepo wachafu.”
Watendakazi Ni Wachache
35 # Mt 4:23 Isa akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi. 36#Mt 15:32; Mk 8:2; 6:34; 1Fal 22:17Alipoona makutano, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. 37#Yn 4:35; Lk 10:2Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. 38#2The 3:1Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu