1
Mahubiri Ya Yahya Mbatizaji
(Mathayo 3:1-12; Luka 3:1-8; Yohana 1:19-28)
1 #
Mt 4:3
Mwanzo wa Injili ya Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu.
2 #
Mal 3:1; Lk 7:27 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:
“Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako”:
3 #
Isa 40:3; Yn 1:23 “sauti ya mtu aliaye nyikani.
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.’ ”
4 #
Yn 1:26, 33; Mt 3:1; Mdo 11:16; Lk 1:7 Yahya alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 5#Mt 3:5Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. 6#Law 11:22; Mt 3:4Yahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 7#Mdo 13:25; Yn 1:27; Mdo 13:25Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. 8#Yoe 2:28; Yn 1:33Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”
Ubatizo Wa Isa
(Mathayo 3:13-17; Luka 3:21-22)
9 #
Mt 2:23; Lk 3:21 Wakati huo Isa akaja kutoka Nasiri ya Galilaya, naye akabatizwa na Yahya katika Mto Yordani. 10#Yn 1:32Isa alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho akishuka juu yake kama hua. 11#Mt 3:17; Mk 9:7; Za 2:7; Isa 42:1Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”
Majaribu Ya Isa
(Mathayo 4:1-11; Luka 4:1-13)
12 #
Mt 4:1; Lk 4:1 Wakati huo huo, Roho akamwongoza Isa kwenda nyikani, 13#Mt 4:10; Ebr 4:15naye akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama wa mwituni, nao malaika wakamhudumia.
Isa Aanza Kuhubiri
14 #
Mt 4:12; 4:23; Mt 4:12; 4:23; Lk 4:14, 15 Baada ya Yahya kukamatwa na kutiwa gerezani, Isa aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, 15#Rum 5:6; Gal 4:4; Mdo 20:21akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”
Isa Awaita Wanafunzi Wanne
(Mathayo 4:12-22; Luka 4:14-15; 5:1-11)
16 #
Mt 4:18; Lk 5:4 Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 17#Mt 13:47Isa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 18#Mt 19:27; Lk 5:11; Mt 4:19Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.
19 #
Mt 4:21
Alipokwenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao. 20Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Isa.
Isa Amtoa Pepo Mchafu
(Luka 4:31-37)
21 #
Mk 1:39; Mt 4:23 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya Sabato, mara Isa akaingia sinagogi, akaanza kufundisha. 22#Mt 7:28-29Watu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana aliwafundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wa sheria. 23#Lk 4:33Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, 24#Mt 8:29; Yn 1:45-46; Mdo 4:10; Za 16:10; 1Yn 2:20naye akapiga kelele akisema, “Tuna nini nawe, Isa Al-Nasiri? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”
25 #
Mk 1:34
Lakini Isa akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” 26#Mk 9:20Yule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa.
27 #
Mk 10:24, 32 Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!” 28#Mk 9:26Sifa zake zikaanza kuenea haraka katika eneo lote la karibu na Galilaya.
Isa Amponya Mama Mkwe Wa Simoni
(Mathayo 8:14-15; Luka 4:38-39)
29 #
Mt 8:14; Lk 4:38 Mara walipotoka katika sinagogi, walikwenda pamoja na Yakobo na Yohana hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. 30Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Isa habari zake. 31#Lk 7:14Hivyo Isa akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia.
Isa Aponya Wengi
(Mathayo 8:16-17; Luka 4:40-41)
32 #
Mt 4:24
Jioni ile baada ya jua kutua, watu wakamletea Isa wagonjwa wote na waliopagawa na pepo wachafu. 33Mji wote ukakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34#Mt 4:23; Mk 3:12; Mdo 16:17-18Isa akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani.
Isa Aenda Galilaya
(Luka 4:42-44)
35 #
Lk 3:21
Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Isa akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. 36#Lk 4:43-44Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta, 37nao walipomwona, wakamwambia, “Kila mtu anakutafuta!”
38 #
Isa 61:1
Isa akawajibu, “Twendeni mahali pengine kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia, kwa sababu hicho ndicho nilichokuja kukifanya.” 39#Mt 4:23-24Kwa hiyo akazunguka Galilaya kote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu.
Isa Amtakasa Mwenye Ukoma
(Mathayo 8:1-4; Luka 5:12-16)
40 #
Mk 10:17
Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Isa, akamwomba akipiga magoti, akamwambia, “Ukitaka, waweza kunitakasa.”
41Isa, akiwa amejawa na huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!” 42Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika. 43#Mk 3:12; 7:36Baada ya Isa kumwonya vikali, akamruhusu aende zake 44#Mt 8:4; Law 13:49; 14:1-32akimwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Musa kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.” 45#Lk 5:15-16, 17; Yn 6:2Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Isa hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi lakini alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande.