15
Isa Mbele Ya Pilato
(Mathayo 27:1-14; Luka 23:1-5; Yohana 18:28-38)
1 #
Mt 27:1-2; Lk 22:66; Mt 5:22 Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Isa, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.
2 #
Mt 2:2
Pilato akamuuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?”
Isa akajibu, “Wewe umesema.”
3Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. 4#Mt 27:13Pilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.”
5 #
Mk 14:61
Lakini Isa hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa.
Pilato Amtoa Isa Asulubiwe
(Mathayo 27:15-26; Luka 23:13-25; Yohana 18:39–19:16)
6 #
Mt 27:15; Lk 23:17; Yn 18:39 Ilikuwa desturi wakati wa Sikukuu ya Pasaka kumfungulia mfungwa yeyote ambaye watu wangemtaka. 7Wakati huo, mtu aliyeitwa Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wametekeleza uuaji wakati wa maasi. 8Ule umati wa watu ukamjia Pilato na kumwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi yake.
9Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie huyu Mfalme wa Wayahudi?” 10#Yn 11:48; 12:19; Mt 27:38Kwa maana yeye alitambua kuwa viongozi wa makuhani walikuwa wamemtia Isa mikononi mwake kwa ajili ya wivu. 11#Mdo 3:14Lakini viongozi wa makuhani wakauchochea ule umati wa watu wamwombe awafungulie Baraba badala yake.
12Pilato akawauliza tena, “Basi mnataka nifanye nini na huyu mtu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?”
13Wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe!”
14Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?”
Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, wakisema, “Msulubishe!”
15 #
Isa 53:6; Mt 27:26; Yn 19:1, 36 Pilato, akitaka kuuridhisha ule umati wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Isa achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.
Askari Wamdhihaki Isa
(Mathayo 27:27-31; Yohana 19:2-3)
16 #
Yn 18:28-33; 19:9 Askari wakampeleka Isa hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio,#15:16 Praitorio maana yake ni makao makuu ya mtawala; ni jumba la kifalme lililokuwa linakaliwa na Pontio Pilato huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu. wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17Wakamvalisha Isa joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani. 18Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” 19Wakampiga kwa fimbo ya mwanzi tena na tena kichwani na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake, wakamsujudia kwa kumdhihaki. 20#Ebr 13:12Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe.
Kusulubiwa Kwa Isa
(Mathayo 27:32-44; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27)
21 #
Mt 27:32; Lk 23:36 Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Iskanda na Rufo, alikuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shamba, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 22#Mt 27:33; Lk 23:33; Yn 19:17Kisha wakampeleka Isa mpaka mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 23#Za 69:21; Mit 31:6Nao wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini hakuinywa. 24#Za 22; 18Basi wakamsulubisha, nazo nguo zake wakagawana miongoni mwao kwa kuzipigia kura ili kuamua ni gani kila mtu ataichukua.
25 #
Mt 27:45; Lk 23:44; Yn 19:14 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26#Mt 27:37; Yn 19:19; Mk 15:2Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: “Mfalme wa Wayahudi.” 27#Mt 27:38Pamoja naye walisulubiwa wanyang’anyi wawili, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. [28#Isa 51:12; Lk 22:37Nayo maandiko yakatimizwa, yale yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na watenda dhambi.]” 29#Za 22:7; Za 109:25; Mk 14:58; Yn 2:19Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao na kusema, “Aha! Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, 30basi shuka kutoka msalabani na ujiokoe mwenyewe!”
31 #
Za 22:7
Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa sheria wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! 32#Mk 14:61; Mk 15:2Basi huyu Al-Masihi,#15:32 Al-Masihi maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. huyu Mfalme wa Israeli, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.
Kifo Cha Isa Msalabani
(Mathayo 27:45-56; Luka 23:44-49; Yohana 19:28-30)
33 #
Amo 8:9
Ilipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa. 34#Za 21:1; Mt 27:46Mnamo saa tisa, Isa akapaza sauti, akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
35Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni anamwita Ilya.”
36 #
Mk 15:23; Za 69:21 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Isa ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Ilya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”
37 #
Yn 19:30
Kisha Isa akatoa sauti kuu, akakata roho.
38 #
Ebr 10:19-20
Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini. 39#Mt 4:3; Mk 9:7Basi yule jemadari aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Isa aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
40 #
Za 38:11; Lk 24:10; Yn 19:25 Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwepo Maria Magdalene, na Maria mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome. 41#Mt 27:55-56; Lk 8:2-3Hawa walifuatana na Isa na kushughulikia mahitaji yake alipokuwa Galilaya. Pia walikuwepo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja pamoja naye Yerusalemu.
Maziko Ya Isa
(Mathayo 27:57-61; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42)
42 #
Mt 27:62; Yn 19:31 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa Siku ya Maandalizi, yaani siku moja kabla ya Sabato, 43#Mt 5:22; Mt 3:2; Lk 2:25, 38Yusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na ambaye alikuwa anautarajia Ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Isa. 44Pilato alikuwa akijiuliza kama Isa alikuwa amekwisha kufa. Hivyo akamwita yule jemadari, akamuuliza iwapo Isa alikuwa amekwisha kufa. 45#Mk 15:39Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. 46#Mk 16:3Hivyo Yusufu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi. 47Maria Magdalene na Maria mamaye Yose walipaona mahali pale alipolazwa.