Marko 16
NMM

Marko 16

16
Kufufuka Kwa Isa
(Mathayo 28:1-8; Luka 24:1-12; Yohana 20:1-10)
1 # Lk 24:9; Yn 19:39-40 Sabato ilipomalizika, Maria Magdalene, Maria mama yake Yakobo, na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Isa. 2#Lk 24:1; Yn 20:1Asubuhi na mapema, siku ya kwanza ya juma, mara tu baada ya kuchomoza jua, walikwenda kaburini. 3#Mk 15:46Njiani wakawa wanaulizana wao kwa wao, “Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe kutoka kwenye ingilio la kaburi?”
4Lakini walipotazama, wakaona lile jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana, limekwisha kuvingirishwa kutoka pale penye ingilio la kaburi. 5#Lk 24:3-4Walipokuwa wakiingia mle kaburini, wakamwona kijana mmoja aliyevaa joho jeupe akiwa ameketi upande wa kuume, nao wakastaajabu.
6 # Mk 1:24 Yule malaika akawaambia, “Msistaajabu. Mnamtafuta Isa, Mnasiri, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa. Tazameni mahali walipomlaza. 7#Yn 21:1-23; Mk 14:28Lakini nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro, kwamba, ‘Anawatangulia kwenda Galilaya. Huko ndiko mtamwona, kama alivyowaambia.’ ”
8 # Mt 28:8; Lk 24:9 Hivyo wakatoka, wakakimbia kutoka mle kaburini wakiwa na hofu kuu na mshangao. Nao hawakumwambia mtu yeyote neno lolote, kwa sababu waliogopa.
Isa Anamtokea Maria Magdalene
(Mathayo 28:9-10; Yohana 20:11-18)
9 # Mk 15:4-7 Isa alipofufuka alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Maria Magdalene, yule ambaye alikuwa amemtoa pepo wachafu saba. 10#Lk 24:10; Yn 20:18Maria akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Isa, waliokuwa wanaomboleza na kulia. 11#Mk 16:13, 14; Lk 24:11Lakini waliposikia kwamba Isa yu hai na kwamba Maria alikuwa amemwona, hawakusadiki.
Isa Awatokea Wanafunzi Wawili
(Luka 24:13-35)
12 # Lk 24:13-32 Baadaye Isa akawatokea wawili miongoni mwa wanafunzi wake walipokuwa wakienda shambani akiwa katika sura nyingine. 13Nao wakarudi na kuwaambia wenzao. Lakini hawakuwasadiki wao pia.
Isa Awaagiza Wale Wanafunzi Kumi Na Mmoja
(Mathayo 28:16-20; Luka 24:36-49; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)
14 # Lk 24:36-43 Baadaye Isa akawatokea wale wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa wakila chakula. Akawakemea kwa kutoamini kwao na kwa ugumu wa mioyo yao kwa kutosadiki wale waliomwona baada yake kufufuka.
15 # Mt 28:18-20; Mdo 1:8 Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16#Mdo 16:31; Yn 12:48Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini yeyote asiyeamini atahukumiwa. 17#Lk 10:17; 1Kor 13:1; 14:2-39Nazo ishara hizi zitafuatana na wanaoamini: Kwa Jina langu watatoa pepo wachafu; watasema kwa lugha mpya; 18#Lk 10:19; Mdo 28:3-5; 6:6watashika nyoka kwa mikono yao; na hata wakinywa kitu chochote cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.”
Isa Apaa Kwenda Mbinguni
(Luka 24:50-53; Matendo 1:9-11)
19 # Lk 24:50-51; Yn 6:6; Mdo 1:19; 1Tim 3:16; Za 110:1; Mt 26:64; Mdo 2:33; 5:31; Rum 8:34; Kol 3:1; Ebr 1:3; 12:2 Baada ya Bwana Isa kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu. 20#Yn 4:48Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu