Nahumu 1
NMM

Nahumu 1

1
1 # Isa 13:1; 19:1; Yer 23:33-34; 50:18; Mwa 10:11; Nah 2:8; 3:7 Neno alilosema Mungu kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono cha Nahumu, Mwelkoshi.
Hasira Ya Mungu Dhidi Ya Ninawi
2 # Kut 20:5; Mwa 4:24; Kum 32:41; 7:10; Za 94:1 Bwana ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi;
Bwana hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu.
Bwana hulipiza kisasi juu ya watesi wake,
naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake.
3 # Neh 9:17; Kut 34:7; 19:16; Za 103:8; Mik 7:18; 2Sam 22:10; Za 50:3; 104:3 Bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu,
Bwana hataacha kuadhibu wenye hatia.
Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani,
na mawingu ni vumbi la miguu yake.
4 # 2Sam 22:16; Kut 14:22; Isa 33:9; Yos 3:15, 16 Anakemea bahari na kuikausha,
anafanya mito yote kukauka.
Bashani na Karmeli zinanyauka
na maua ya Lebanoni hukauka.
5 # Kut 19:18; Ay 9:6; 2Sam 22:8; Yoe 2:10; Eze 38:20; Mik 1:4 Milima hutikisika mbele yake
na vilima huyeyuka.
Nchi hutetemeka mbele yake,
dunia na wote waishio ndani yake.
6 # Za 130:3; Eze 22:14; Isa 5:24-25; 42:25; Yer 10:10; 1Fal 19:11 Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu?
Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali?
Ghadhabu yake imemiminwa kama moto,
na miamba inapasuka mbele zake.
7 # Yer 33:11; 17:17; Za 22:9; 1:6; 2Tim 2:19 Bwana ni Mwema,
kimbilio wakati wa taabu.
Huwatunza wale wanaomtegemea,
8 # Isa 8:7; Amo 8:8; Dan 9:26 lakini kwa mafuriko makubwa,
ataangamiza Ninawi;
atafuatilia adui zake hadi gizani.
9 # Hos 7:15 Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya Bwana
yeye atalikomesha;
taabu haitatokea mara ya pili.
10 # 2Sam 23:6; Isa 49:26; 5:24; Mal 4:1 Watasongwa katikati ya miiba
na kulewa kwa mvinyo wao.
Watateketezwa kama mabua makavu.
11Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja,
ambaye anapanga shauri baya
dhidi ya Bwana
na kushauri uovu.
12 # Isa 10:34; Isa 54:6-8; Mao 3:31-32 Hili ndilo asemalo Bwana:
“Ingawa wana muungano nao ni wengi sana,
watakatiliwa mbali na kuangamia.
Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda,
sitakutesa tena.
13 # Isa 9:4; Ay 12:18; Za 107:14 Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako,
nami nitazivunjilia mbali pingu zako.”
14 # Isa 14:22; Mik 5:13; Yer 28:8; Eze 32:22-23 Hii ndiyo amri Bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi:
“Hutakuwa na wazao
watakaoendeleza jina lako.
Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha
ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu.
Nitaandaa kaburi lako,
kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”
15 # Isa 40:9; Rum 10:15; Isa 52:7; Mdo 10:36; Law 23:2-4 Tazama, huko juu milimani,
miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema,
ambaye anatangaza amani!
Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako,
nawe utimize nadhiri zako.
Waovu hawatakuvamia tena;
wataangamizwa kabisa.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu