3
Ole Wa Ninawi
1 #
Eze 22:2; Mik 3:10; Za 12:2 Ole wa mji umwagao damu,
uliojaa uongo,
umejaa nyara,
usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara.
2 #
Isa 34:3; Yer 47:3 Kelele za mijeledi,
vishindo vya magurudumu,
farasi waendao mbio
na mshtuo wa magari ya vita!
3Wapanda farasi wanaenda mbio,
panga zinameremeta,
na mikuki inang’aa!
Majeruhi wengi,
malundo ya maiti,
idadi kubwa ya miili isiyohesabika,
watu wanajikwaa juu ya mizoga:
4 #
Isa 47:9; 23:17; 2The 2:9, 10; Dan 2:2; Ufu 9:20, 21; Eze 16:25-29 yote haya kwa sababu ya wingi wa tamaa za kahaba,
anayeshawishi, bibi wa mambo ya uchawi,
anayewatia utumwani mataifa kwa ukahaba wake
na pia jamaa za watu kwa ulozi wake.
5 #
Nah 2:13; Isa 47:2-3; 20:4; Yer 13:22 Bwana Mwenye Nguvu Zote anasema,
“Mimi ni kinyume na ninyi.
Nitafunika uso wako kwa gauni lako.
Nitaonyesha mataifa uchi wako
na falme aibu yako.
6 #
Kut 29:14; Ay 9:31; 1Sam 2:30; Yer 51:37; Isa 14:16 Nitakutupia uchafu,
nitakufanyia dharau
na kukufanya kioja.
7 #
Isa 13:14; 31:9; Nah 1:1; Ay 3:14; Yer 51:37 Wote wanaokuona watakukimbia na kusema,
‘Ninawi ipo katika kuangamia:
ni nani atakayeomboleza kwa ajili yake?’
Nitampata wapi yeyote wa kukufariji?”
8 #
Amo 6:2; Yer 46:25; Isa 19:6-9 Je, wewe ni bora kuliko No-Amoni,
uliopo katika Mto Naili,
uliozungukwa na maji?
Mto ulikuwa kinga yake,
nayo maji yalikuwa ukuta wake.
9 #
Mwa 10:6; 2Nya 12:3; Eze 27:10; 30:5 Kushi#3:9 Kushi ni Ethiopia. na Misri walikuwa nguvu zake zisizo na mpaka;
Putu na Libia walikuwa miongoni mwa wale walioungana naye.
10 #
Isa 20:4; 2Fal 8:12; Isa 13:16; Hos 13:16; Ay 6:26-27; Eze 24:6; Yer 40:1; Yoe 3:3; Oba 1:11 Hata hivyo alichukuliwa mateka
na kwenda uhamishoni.
Watoto wake wachanga walivunjwa vunjwa vipande
kwenye mwanzo wa kila barabara.
Kura zilipigwa kwa watu wake wenye heshima,
na watu wake wote wakuu walifungwa kwa minyororo.
11 #
Isa 49:26; 2:10 Wewe pia utalewa;
utakwenda mafichoni
na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui.
12 #
Wim 2:13; Ufu 6:13; Isa 28:4 Ngome zako zote ni kama mitini
yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva;
wakati inapotikiswa,
tini huanguka kwenye kinywa chake alaye.
13 #
Isa 19:16; 45:2; Yer 50:37; Nah 2:6 Tazama vikosi vyako:
wote ni wanawake!
Malango ya nchi yako
yamekuwa wazi kwa adui zako;
moto umeteketeza mapingo yake.
14 #
2Nya 32:4; Nah 2:1 Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako,
imarisha ulinzi wako,
Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi,
yakanyage matope,
karabati tanuru la kuchomea matofali!
15 #
Isa 27:1; 2Sam 2:26; Yer 51:14; Yoe 1:4 Huko moto utakuteketeza,
huko upanga utakuangusha chini
na kama vile panzi, watakumaliza.
Ongezeka kama panzi,
ongezeka kama nzige!
16 #
Kut 10:13
Umeongeza idadi ya wafanyabiashara wako
mpaka wamekuwa wengi kuliko nyota za angani,
lakini kama nzige wanaacha nchi tupu
kisha huruka na kwenda zake.
17 #
Ufu 9:7; Yer 51:17 Walinzi wako ni kama nzige,
maafisa wako ni kama makundi ya nzige
watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi:
lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao,
na hakuna ajuaye waendako.
18 #
Za 76:5-6; Yer 25:27; 50:18; Eze 31:3; Isa 56:10; 1Fal 22:17 Ee mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wanasinzia;
wakuu wako wanalala chini mavumbini kupumzika.
Watu wako wametawanyika juu ya milima
bila kuwa na mtu yeyote wa kuwakusanya.
19 #
Yer 30:13; Mik 1:9; Ay 27:23; Mao 2:15; Sef 2:15; Isa 14:8; 37:18 Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako;
jeraha lako ni la kukuua.
Kila anayesikia habari zako,
hupiga makofi kwa kuanguka kwako,
kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa
na ukatili wako usio na mwisho?